Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col. Evance Mallasa akiambatana na Katibu tawala Wilaya na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ameongoza kikao cha Maji na Usafi wa Mazingira (WASH) ambacho kimehusisha wadau mbalimbali Wilaya ya Kakonko Kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko leo tarehe 9 Januari 2025.
Kikao ichi Kuilihuisisha Wataalamu Kutoka Halmashauri pamoja na wadau Mbalimbali wakiwemo UNICEF, Red-Cross, World Vision Tanzania na Water Mission. Ambapo Mada kubwa iliyojadidiliwa katika kikao hicho ni namna utekelezaji wa programu ya WASH inavyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.
Wakati wakiendelea na kikao hicho Col. Mallasa ameeleza kuwa kikao hicho ni muhimu na kuwaelekeza suala la usafi wa mazingira kuwa agenda ya kudumu katika vikao. Hivyo wananchi wanahitaji uhamasishaji na uelimishaji wa kutosha ili waweze kutekeleza shughuli za usafi wa mazingira na kuleta tija kama ilivyokusudiwa.
Aidha ameendelea kusistiza idara ya afya kwa kushirikiana na Halmashauri kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa vyoo bora,namna ya kuhifadhi taka ngumu na taka laini pamoja na kuwataka wananchi kudumisha usafi katika mazingira yanayowazunguka.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Kakonko Ndg.Maulid Mtulia,amesisitiza juu ya ushirikishwaji wa jamii na viongozi ngazi zote ili kuboresha mazingira yanayowazunguka na pia amesisitiza uwepo wa vifaa vya kuhifadhia taka katika maeneo yote ya umma.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Dkt. Godfrey Kayombo amewasisitiza wataalamu kutoka Halmashauri kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia miongozo, sera na taratibu za Serikali ili kutimiza wajibu wao.
Mbali hayo Wadau walioshiriki katika kikao hicho wameahidi kuiunga mkono Serikali katika jitihada za kuboresha Afya, maji na mazingira katika jamii na Kuwaomba wananchi kuendelea kushiriki na kuwaunga mkono wadau katika utekelezaji wa shughuli hizi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa