Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa amewataka wahitimu 134 waliofuzu mafunzo ya mgambo kwa mwaka 2022 kutumia mafunzo hayo kwa manufaa ya nchi na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.
“Niwaase kitu kimoja mnapohitimu mkaridhike na hali zenu msijihuishe na uhalifu kwa kutumia mafunzo miliyoyapata, alisema Col.Mallasa.
Col.Mallasa ameyasema hayo siku ya Jumanne tarehe 25 Oktoba, 2022 wakati akifunga mafunzo ya jeshi la mgambo kwa wahitimu 134 waliofuzu kati ya 290 katika Kijiji cha Kinyinya kata ya Nyamtukuza Wilayani Kakonko.
Mafunzo hayo yalianza tarehe 1 Juni, 2022 kwa wanafunzi 290 ambapo wanaume walikuwa 275 na wanawake 15 lakini waliohitimu mafunzo ni 134 ambapo wanaume ni 128 na wanawake 06.
Wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wahitimu hao wameeleza wamesoma masomo 07 yakiwemo kwata, silaha, usalama wa raia, kuzuia na kupambana na rushwa, huduma ya kwanza, ukakamavu wa mwili na uraia.
Aidha katika kipindi cha mafunzo wahitimu walishiriki na kuchangia shughuli za jamii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Kuchangia damu, kufanya usafi kituo cha afya Nyanzige na hospitali ya Wilaya siku ya mashujaa , kuchoma tofali 6000 sawa na 900,000 na kutoa hamasa kwa Wananchi katika ziara ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Wilayani Kakonko tarehe 16 Oktoba, 2022.
Wahitimu hao wamekabidhi tofali 6000 kwa Mgeni rasmi ambaye naye alikabidhi matofali hayo 6000 kwa Mtendaji wa Kijiji cha Kinyinya ili yatumike katika shughuli za kijamii zinazoendelea katika kijiji hicho kilichopo katika kata ya Nyamtukuza Wilayani Kakonko.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa