Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa ametoa siku tano kuanzia siku ya Alhamisi tarehe 12 Januari 2023, Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wawe wameripoti kwenye shule walizopangiwa.
Col.Mallasa ameeleza kuwa amefanikiwa kufanya ziara ya ukaguzi wa madarasa katika shule za 10 kati ya shule 15 za Sekondari Wilayani Kakonko nakubaini kuwa wanafunzi walio ripoti Shuleni mpaka sasa ni wachache takribani wanafunzi 302 kati ya wanafunzi 2260 waliotakiwa kusajiliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa Waratibu Elimu wote, Watendaji wa Kata na Vijiji kuanzia tarehe 17 Januari 2023, kuendelea kutoa Elimu kwa wazazi juu ya umuhimu wa Elimu na kuhakikisha Wanafunzi wanafika Shule kwa wakati.
Aidha amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara husika kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wazazi ambao watakaidi agizo hilo ili kuhakikisha Watoto wanakwenda Shule kwa wakati.
“Tunataka kuona wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaenda shule kwa wakati na masomo yanaanza haraka kwani ujenzi wa madarasa umekamilika kwa asilimia kubwa na mengine yapo katika hatua ya ukamilishaji”, Alisema Col.Mallasa.
Mkuu wa Wilaya amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa milioni 760 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 38 katika Wilaya ya Kakonko.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa