Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa amewataka Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Kigoma kuzingatia utoaji wa fidia kwa Wananchi watakaopitiwa na mradi wa barabara ya lami wakati wa kufanya tathmini za maeneo ya Wananchi wa Kata ya Mugunzu iliyopo Wilayani Kakonko.
Amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mugunzu Wilayani Kakonko kiijiji cha Kiduduye, Kiniha, Nyagwijima na Mugunzu wakati wa ziara yake Januari 16-17,2023, amewasisitiza wakala wa barabara kuhakikisha wanazingatia utoaji wa fidia kwa wakati kwa Wananchi ambao watapitiwa na mradi wa ujenzi wa barabara.
Ameendelea kusema mradi wa ujenzi wa barabara utasaidia kuwepo kwa fursa mbalimbali za ajira kwa vijana wa Kata ya Mugunzu ambazo zitawasaidia kujiimarisha kiuchumi. Hivyo barabara itakapokamilika kwa kiwango cha lami usafiri na usafirishaji utakuwa rahisi na maendeleo yatapatikana kwa kiwango cha juu.
Aidha ametoa angalizo kwa wananchi wa Kata ya Mugunzu kuwa makini wanapokua barabarani ili kuepuka ajali zitakazoweza kusababisha ulemavu wa kudumu au kupoteza Maisha wakati ujenzi utakapoanza
Kanali Mallasa ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuendelea kujenga na kuimarisha miundombinu ya ujenzi wa barabara, madarasa na nyumba za walimu.
Kwa upande wake mthamini kutoka TANROADS Mkoa wa Kigoma ndugu Mihayo Ezekiel amesema lengo la utoaji Elimu ni kuutambulisha mradi kwa wananchi wa kata ya Mugunzu na kutambua taratibu za utoaji wa fidia kwa Wananchi ambao mradi utapita katika maeneo yao, hivyo amewaomba Wananchi kuupokea mradi huo kwani utaleta mabadiliko chanya kwa kutoa fursa za ajira na kuraisisha shughuli za kibiashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Wananchi wa Kata ya Mugunzu wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupeleka mradi wa barabara ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami kutoka Kibondo kupitia Mugunzu mpaka Mabamba kwani itawasaidia katika shughuli za kiuchumi hasa biashara kwani shughuli kubwa ya wana Mugunzu ni kilimo hivyo itakuwa rahisi kusafirisha mazao kwenda Sokoni kwa wakati nakupelekea kukua kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa