Jina la Twiga linasadikika kutokana na maneno ya Kiarabu "ziraafah" (Mkusanyiko na mwonekano wa madoa doa), "zirafah" (Mrefu zaidi) na "xirapha" ("Mwepesi katika kutembea"), pia katika lugha ya Kiingereza "camelopard" na kiafrikana "kameelperd" (Chui kama ngamia).
Leo tarehe 17 Juni, 2023 tunaadhimisha siku ya Twiga duniani, mnyama mrefu zaidi kuliko wanyama wote watembeao nchi kavu katika uso wa dunia. Twiga ni mnyama wa kipekee sana na anastahili kuwa mnyama wa taifa la Tanzania.
Urefu wa mpaka mita 5.5 huwaruhusu Twiga kula matawi juu ya miti yasiyoweza kufikiwa na wanyama wengine wote isipokuwa Tembo, jambo ambalo humsaidia Twiga kupunguza ushindani katika kutafuta chakula.
Hata hivyo Twiga anapokuwa anakula matawi na maua ya miti, husaidia katika uchavushaji wa maua (pollination), hususani miti aina ya knob thorn "acacia nigrescens".
Maisha na kesho ya wanyama mbugani mara nyingi huamuliwa kwa kuona kabla ya kuonekana. Urefu wa twiga na uwezo mzuri wa macho katika kuona huwawezesha kuona umbali mrefu na kukagua maeneo yao ili kuepuka wanyama wanaowinda. Hii hupelekea wanyama wengine kupenda kujumuika na twiga katika kutafuta malisho wakiwa na uhakika wa hali ya usalama zaidi.
Twiga ni mnyama mtaratibu sana na hupendelea kuepukana na hatari iliyopo mbele yake kwa kuamua kuondoka eneo hilo. Hivyo basi ni jukumu letu sote kulinda na kutunza tunu hii ya taifa la Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa