Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col. Evance M. Mallasa amezindua mpango mkakati wa unawaji mikono na na kusisitiza huduma za kunawa ziwekwe maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu.
“Huduma za kunawa mikono ziwepo na maji yawekwe kwenye ofisi, Nyumba za Ibada, Shule, Masoko, Hospitali, sehemu za stsrehe na sehemu zote zenye mikusanyiko ya watu”, alieleza Col.Evance Mallasa.
uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko tarehe 4 Novemba 2022, lengo ikiwa ni kupunguza magonjwa ya kuambukizwa hususani kwa watoto wadogo.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameagiza RUWASA kuhakikisha maji yanapatikana maeneo mbalimbali huduma zinapotolewa ili Wananchi waweze kudumisha Afya kwa kunawa mikono na kupunguza maambukizi ya magonjwa kutokana na uchafu.
Kwa upande wa familia Col.Mallasa amesisitiza mkuu wa Kaya hususani wanaume wahakikishe huduma ya maji inafika nyumbani ili kulinda afya ya familia nzima kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF) imezindua mpango mkakati wa unawaji Mikono (Roadmap to universal hand hyagiene).
Wajumbe mbalimbali wamehudhuria uzinduzi wa mpango mkakati wa unawaji mikono wakiwemo kamati ya Usalama ya Wilaya, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa divisheni na vitengo, Watendaji wa kata na Viongozi wa dini.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa