Leo Alhamisi Novemba 7, 2024, Msimamizi wa Uchanguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Ndaki Stephano Mhuli amekutana na Viongozi vya Vyama vya Siasa 07 Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata pamoja na Wajumbe wa timu ya Uratibu Wilaya kwa lengo la kujadiliana ili kuongeza Vituo 16 vya kupigia kura.
Akizungumza na Viongozi hao kutoka chama cha Mapinduzi (CCM), UDP, CHADEMA,CHAUMA,CUF,ACT,NCCR MAGEUZI,katika Ukumbi wa Gombe uliopo ofisi za Halmashauri Kakonko, Msimamizi wa Uchaguzi, ameeleza kuwa kutokana na wingi wa wapiga kura ambapo vituo hivyo 16 vilivyoongezwa vina wapiga kura kuanzia 400 hadi 800 ina kuwa ni vigumu wote kupiga kura na kuisha kufikia saa 10 jioni ambayo ni muda wa mwisho wa kupiga kura kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi wa Serikali za mita kwa mwaka 2024.
Ameongeza kuwa ili kupunguza foleni ya watu na muda wa kupiga kura vituo hivyo 16 vitaongezwa maeneo yaleyale ambayo yana vituo vya awali vya kupigia kura akitolea mfano kwa vituo ambavyo vipo shuleni yatatumika madarasa mawili badala ya moja ili kufikia wapiga kura wote wakati kwa upande wa vituo vya wazi wataongeza hema karibu na kituo cha mwanzo na kuongeza wasimamizi wa vituo.
Aidha wajumbe wameridhia na kupongeza kwa hatua hiyo ya Msimamizi wa Uchaguzi aliyoifanya kwani ina nia njema pia wameomba wapewe maandishi mapema kwani itawasaidia kuongeza mawakala.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika Novemba 27 Mwaka huu pia Kampeni zinatarajia kuanza tarehe 20-26,2024.
Kauli mbiu. ‘’Serikali za Mitaa,Sauti ya Wananchi Jitokeze kushiriki Uchaguzi’’.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa