Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa 2022 zimefanyika Wilayani Kakonko tarehe 05 Oktoba, 2022 na kutembelea miradi 06 yenye thamani ya Tshs. 1,198,752,565.00.
Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2022 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa ameeleza kuwa shughuli itakayofanyika kwenye miradi 06 ni kuweka jiwe la Msingi katika Kituo cha Afya Mugunzu kinachojengwa kwa thamani ya Tshs.517,350,000, Kutembelea Klabu ya Wapinga rushwa katika shule ya Sokondari Gwanumpu, Kuzindua kisima cha maji Nyakayenzi chenye thamani ya Tshs.436,530,220, Ufunguzi wa Zahanati ya Kihomoka iliyojengwa kwa mapato ya ndani kwa thamani ya Tshs.74,386,700, Uzinduzi wa bweni katika shule ya Sekondari ya Wasichana Kakonko iliyopo kata ya Kanyonza kwa thamani ya Tshs.130,689,645 na kutembelea kikundi cha Vijana Tuinuane – Muganza chenye mradi wa kukamua mafuta ya alizeti na kusindika wenye juimla ya Tshs.39,796,000.
Mwenge wa Uhuru umeridhia miradi yote 06 Wilayani Kakonko na kukabidhiwa kimkoa Mkoani Kagera tarehe 06 Oktoba, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andegenye.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa