Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Abdalla Shaib Kaim ameridhishwa na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo aliyoikagua, kutembelea , Kuweka Mawe ya Msingi na Kuzindua Katika Wilaya ya Kakonko.
Miradi hiyo ni Shule ya Sekondari Kakonko Wasichana, Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya (Ikulu Ndogo), kiwanda cha kutengeneza Mkaa Mbadala, Barabara ya Lami yenye Kilomita 1.3 Kakonko - Itumbiko, Zahanati ya Kijiji cha Ilabiro, Ofisi ya Afisa Tarafa Kasanda, Kikundi cha Vijana Azimio, Klabu ya Wapinga Rushwa Buyungu Sekondari na Shamba la miti iliyopandwa kijiji cha kiga.
Aidha Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameeleza matokeo mazuri ya ukaguzi wa miradi yanatokana na usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa Viongozi wa Mkoa kuanzia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma CGF (Rtd) Thobias Andengenye, Katibu Tawala Mkoa Mhe. Albert Msovela na Mhandisi wa Mkoa Fransicso Magoti.
Amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa kwa Juhudi na kazi nzuri aliyoifanya katika miradi, vile vile amewapongeza Wakurugenzi Watendaji Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Wakuu wa Taasisi,Mashirika ,Waheshimiwa Madiwani, Mwenyekiti wa CCM Wilaya na Vyama Vingine Vya Siasa pamoja na Wananchi wote kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa ipasavyo.
Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameelekeza maeneo yote yaliyobainika kuwa na dosari yarekebishwe kwa muda uliopangwa na baada ya marekebisho itumwe video na picha ya baada na kabla pamoja na viambata vya fedha ambazo zilikua hazijalipwa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa