Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga amewahimiza wakulima wa pamba Wilayani Kakonko kulima pamba kwa ubora na kuimarisha ushirika ili kuongeza uchumi kwa kila mtu. Akifanya ziara Wilayani kakonko hivi karibuni kuhasisha kilimo bora cha pamba mhe.Maganga ameeleza kuwa Serikali imetoa ruzuku na bei elekezi kwa mbolea ya kupandia ya DAP ambayo itauzwa Tsh.55741 na mbolea ya kukuzia UREA itauzwa Tsh.43,162. Hapo awali mbolea hizo zilikuwa zikiuzwa kati ya sh.50,000 hadi 80,000.
Aidha mkuu wa Mkoa amewaagiza Maafisa ugani kulima mashamba ya mfano ili wananchi waweze kujifunza kupitia mashamba hayo. Wakati huo amesisitiza suala la utii wa sheria bila shuruti ikiwemo kuepuka kilimo cha bangi ambapo mwaka jana 2016 heka 8 za bangi zilikamatwa. Vilevile amewataka wananchi kudumisha ushirikiano na upendo na kuacha ukabila. Ameeleza kuwa baadhi ya wananchi wanajichukulia sheria mkononi kwa kuwaua wazee kwa imani za kishirikina.
Aidha ametoa wito kwa wakimbizi wanaoishi nchini Tanzania kuishi kwa amani na watanzania na kuepuka kufanya mauaji na vitendaji vya uporaji. Mkuu wa Mkoa ametembelea kata ya Kasanda, Kanyonza na Kasuga na kuzungumza na wakulima wa pamba ili kuwaeleza mkakati madhubuti wa Serikali kuhakikisha zao la pamba mkoani Kigoma linakuwa na tija zaidi na fida kwa wakulima.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa