Watalamu mbali mbali kutoka kutoka Wilaya ya Kakonko, Kibondo, Kasulu na Kasulu Mji Mwanzoni mwa mwezi February 03,2023 wamekutana katika Ukumbi wa Fitina lay uliopo katika Halmashauri ya Mji Wilayani Kasulu katika Mafunzo ya siku moja kwa lengo la kuwajengea uwezo Wasimamizi na Wawezeshaji wa Programu ya IPOSA.
Wajumbe waliohudhuria Mafunzo hayo ni pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri husika, Maafisa Elimu Msingi, Maafisa Mipango, Maafisa ugavi na Manunuzi, Maafisa maendeleo ya jamiii, Wadau wa Elimu, Viongozi wa Taasisi, Viongozi wa Mashirika ya yasiyo ya kiserikali pamoja na wathibiti ubora wa Shule.
Mgeni rasmi wa Mafunzo hayo Kanali Isack Mwakisu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu wakati alipokaribishwa kufungua mafunzo alieleza programu ya IPOSA inaleta tija kwa vijana kwa sababu vijana wanapofundishwa kwa vitendo ni rahisi kuelewa ukitofautisha na wanavyofundishwa darasani kwani unaweza ukawa umesoma sana lakini ukashindwa kubadili Elimu yako Kuwa Fedha.
“Niwaombe muendelee kuwasisitiza sana hawa vijana kuingia katika prograamu ya IPOSA kwani vijana wengi wapo mtaani wamekata tamaa kwa sababu mbalimbali najua vijana pia wana mambo ya kutaka kupata hela kwa haraka sana bila ya kufanya kazi kwa muda siyo wavumilivu sana lakini sisi ndiyo tunatakiwa kuwa magari yao ya kuwaongoza, sisi tuwe taa tuwaite tuwaeleweshe ili wajiunge na programu ya IPOSA ili waweze kunufaika na kile Serikali inachokilenga kutoka kwa wadau wetu wa maendeleo. Alisema Mwakisu”
Aliendelea kusema wawezeshaji na wasimamizi wa programu ya IPOSA ili kuongeza chachu ya usalama wa vijana kufanya kazi na kujiongezea kipato anahimiza wawafundishe vijana hao namna ya kutumia pesa wanazozipata maana wasiwezeshwe tu namna ya stadi za ufundi mbalimbali bali wawafundishe namna ya kutafuta masoko na ujasiliamali.
Naye Dollar Rajabu Kusenge Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kasulu Mji alisema Halmashauri ya Mji Kasulu imekua ikiendesha fani mbambali kwa vijana ambao wako nje ya mfumo rasmi wa Elimu na yeye ni shahidi wa matokea chanya na makubwa kutoka katika programu ya IPOSA kwa vijana ambao wapo katika programu hiyo.
Aidha aliwashukuru sana wadau wa mbalimbali wa programu ya IPOSA na kuwaomba kuwasaidia vijana ambao wanahitimu mafunzo ya IPOSA na Vyuo vingine vya ufundi kuangalia namna ya kuwawezesha kupata mashine za kisasa wakati wanapokuwa wanajifunza.
Kwa upande wake Siafu Sempeho Mratibu wa Mradi wa programu ya IPOSA Nchini ameeleza kuwa programu ya IPOSA imeanzishwa na Serikali kwa malengo ya kutoa fursa ya Elimu kwa vijana ambao wako nje ya mfumo rasmi wa Elimu. Vijana hao ni wale ambao hawana ujuzi wowote kwani wanafundishwa stadi mbalimbali za Elimu, ufundi, ujasiliamali pamoja na stadi za maisha.
Aidha alieleza kazi ya Wasimamizi na wawezeshaji wa vituo vya programu ya IPOSA ni kuwasaidia vijana kutambua fursa ambazo zipo katika maeneo yao pia kuwasaidia kuunda vikundi vya ‘’IPOSA Empowerment Clubs’’kwani vikundi hivyo vinatakiwa kusajiliwa na kutambuliwa kama viwanda vidogo vidogo ili viweze kupatiwa mafunzo.
‘Lengo kuu la programu ya IPOSA ni kuionyesha Dunia kuwa kijana anaweza kutoka mtaani katika makundi ya uhalifu na akajiunga katika programu ya Serikali na kupatiwa mafunzo bure pia baada ya Mwaka mmoja anauwezo wa kusajiliwa katika kikundi. Alisema Siafu.’’
Mafunzo ya programu ya IPOSA yanaendeshwa na Taasisi ya Elimu ya watu Wazima kupitia Wizara ya Elimu Sanyansi na Teknolojia kwa ufadhili wa Shirika la UNICEF.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa