Wataalamu mbalimbali kutoka ngazi ya Mkoa na Halmashauri kutoka Mikoa ya Kigoma na Kagera mwishoni mwa wiki hii Disemba 22-23, 2022, Wamekutana katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu katika mafunzo ya siku mbili (02) yaliyoandaliwa na OR-TAMISEMI kwa lengo la kuzijengea uwezo Timu za utekelezaji katika mradi mpya wa BOOST.
Wajumbe waliohudhuria Mafunzo hayo ni pamoja na Maaafisa Elimu Msingi, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Wahandisi, Wahasibu, Walimu Wakuu, Maafisa Manunuzi, Wathibiti ubora wa Shule, Maafisa Ustawi wa Jamii na Maafisa Mawasiliano Serikalini.
Mgeni rasmi wa Mafunzo hayo Bi.Paulina Ndigeze Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma wakati akihutubia washiriki wa Mafunzo amewataka kuzingatia mafunzo hayo na kila mmoja akashiriki nafasi yake vizuri katika utekelezaji wa mradi wa BOOST.
Aidha Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka OR-TAMISEMI Ndugu George Jackson amesema mradi wa BOOST unatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitano (05) kwa mwaka 2021/2022 hadi mwaka 2025/2026 kwa fedha za kitanzania Trillioni 1.15 sawa na dora za kimarekani Millioni mia tano.
Amesema Katika Fedha hizo dora za kimarekani Millioni 480 zitatumika katika programu ya lipa kulingana na matokeo na dora za kimarekani millioni 20 zitatumika katika utekelezaji wa miradi.
Ameendelea kusema lengo kubwa la mradi wa BOOST ni kuinua Elimu ya Awali na Msingi kwa Tanzania Bara ambapo jumla ya vyumba vya madarasa elfu 12,000 vinatarajiwa kujengwa, ununuzi wa vifaa vya TEHAMA kwenye Shule za Awali na Msingi pamoja na vituo vya Walimu, Kuongeza kasi ya uandikishaji wa Wanafunzi wa Elimu ya Awali na msingi na uandaaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Malengo mengine ya mradi wa BOOST ni pamoja na kutekeleza Mafunzo endelevu ya Walimu kazini (MEWAKA) na Halmashauri Kusimamia utawala bora katika Elimu kwa kuzingatia miongozo na usimamizi wa Shule.
Amehitimisha kwa kusema Shule za Msingi elfu sita 6000 zitawezeshwa kutekeleza programu Shule ya Msingi salama na tayari mradi wa BOOST umeanza kutekelezwa nchini Tanzania katika Mikoa ya Tanzania bara.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa