Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu Thobias Andengenye amekabidhi kilo 5184 za mahindi na bati 1000 kwa kaya 216 walioathiriwa na mvua na upepo ulionyesha Januari 20,2024 Wilayani Kakonko.
Akikabidhi pole hiyo kwa wana kaya kutoka Vijiji 7 vilivyoathirika na mvua ambavyo ni Kakonko, Mbizi, Itumbiko, Muganza, Chilambo, Nyagwijima na Kiga ameeleza kuwa Rais wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa pole kwa Wakazi wa Wilaya ya Kakonko walioathiriwa na mvua na kuonesha namna anavyowajali.
Aidha amewasisitiza Wananchi kujitokeza kugombea, kupiga kura na kuchagua katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu 2024.
Halfa ya kukabidhi vifaa hivyo vya maafa imefanyika nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa na kuhudhuria na wajumbe wa kamati ya maafa ya Wilaya, kamati ya Usalama, Viongozi wa dini, vyama, wadau mbalimbali pamoja na Wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha moyo wa kujali Wananchi wake hususani wa Wilaya ya Kakonko.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa