Kaimu Meneja msaidizi wa Shirika la Danish Refugee Council (DRC) kitengo cha boresha maisha na Mazingira Bwana Alex Bundala amemkabidhi pikipiki Michael Faraay Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Mwishoni mwa wiki hii 22 disemba, 2022, Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, lengo la utoaji wa pikipiki hiyo ni kuwawezesha Maafisa Maliasili usafiri na urahisi wa ukaguzi wa miradi ya Mazingira na kutoa Elimu kwa Wananchi na Wadau juu ya upandaji wa miti na utunzaji wa Mazingira.
Kwaupande wake Michel Faaray amewashukuru Viongozi wa Shirika la DRC kwa kuendelea kutoa msaada kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, pia ameliomba Shirika kuendelea kushirikiana na viongozi wa ngazi ya Kata na Vijiji ili kuhakikisha Wananchi wanapanda miti katika maeneo yao kwa kuwaelimisha juu ya utunzaji wa Mazingira.
Naye Amani A. Kanguye Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kakonko amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kuonyesha ushirikiano wa kutunza Mazingira na kuwapatia Elimu Wananchi juu ya utunzaji wa Mazingira kwa kuhakikisha Mazingira yanakuwa safi na salama.
Allan Tomas Kutoka kitengo cha manunuzi na ugavi amesema Shirika la DRC litaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhamasisha utunzaji wa Mzingira, kuwezesha usimamizi na uhifadhi wa Mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Taasisi za Serikali zinazojihusisha na utunzaji wa Mazingira.
Aidha Afisa Maliasili na Hifadhi ya Mazingira Wilaya ya Kakonko Bosco Huruma amesema pikipiki hiyo itasaidia katika usafiri na kuiwezesha Idara ya Maliasili kutoa huduma maeneo yote ambayo yana shughuli za uhifadhi wa Mazingira na upandaji wa miti kwani maeneo mengine yalikuwa hayafikiki kutokana na changamoto ya usafiri hivyo kwa sasa maafisa Maliasili wataweza kufika katika maeneo kwa wakati lengo ikiwa nikuwawezesha Wananchi na kuwaelimisha juu ya upandaji wa miti na uhifadhi wa Mazingira.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa