Mkuu wa Shirika la UNHCR kibondo Mkoani Kigoma Henok Ochalla amemkabidhi Jonas Joas Afisa Elimu Mkoa Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Nyaraka za Vyumba viwili( 02) vya Madarasa ,Majengo Mawili (02) ya Vyoo vya Wasichana na Wavulana Vyenye Matundu Sita ( 06) ,pamoja na matanki mawili ya maji ( 02) yenye lita 5000, Katika Shule ya Msingi Nyanzige iliyopo kata ya Nyamtukuza Wilayani Kakonko leo disemba 15,2022.
Aidha Jonas Joas nae amemkabidhi Christopher Bukombe Afisa Elimu Sekondari Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Nyaraka za Majengo Hayo na kuwahimiza Wananchi kuitunza na kuilinda Miundombinu hiyo ili Wanafunzi wapate Elimu Katika Mazingira Bora.
Madarasa hayo na Vyoo yamejengwa kwa ufadhili wa Shirika la UNHCR na kugharimu kiasi cha Tsh.Millioni Mia Moja na Thelathini na Nne Laki Saba Elfu ishirini na Mia Nne Themanini na Mbili(134,720,482).
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa