Mratibu wa Miradi ya Kasanda na Nyaronga Area Programme Bi.Bertha Mtesigwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Shirika la World Vision Ndg. James Angawa Anditi na Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Kigoma Ndg.Mkama Nangu amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa miradi (13) katika sekta ya Afya na Elimu yenye thamani ya Tshs.1,067,031,234/= (Bilioni Moja na Milioni sitini na Saba) katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika kata ya Nyamtukuza kijiji cha Churazo leo Agosti 11,2023.
Bi. Bertha ameeleza miradi hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2021-2022 ambayo ni Zahanati ya Chilambo kwa gharama ya Tshs. 157,000,000/=, ukarabati wa Jengo la OPD Nyanzige kwa gharama ya Tshs.145,000,000/=, Vyoo matundu 12(6 ke, 6me)shule ya msingi katanga. kwa gharama ya Tshs.68,000,000/=, Zahanati ya Ilabiro OPD,RCH,Maternity and Delivery unity kwa gharama ya Tshs.207,286,687/=, Matundu (4) ya vyoo Zahanati ya Ilabiro kwa gharama ya Tshs.27,794,546/=,Zahanati ya Churazo OPD,RCH,Maternity and Delivery unity kwa gharama ya Tshs.209,276,132/=, Matundu (2) ya Vyoo Zahanati ya Churazo kwa gharama ya Tshs. 20,723,868/=, Incenerator na Placenta Pit Zahanati ya Ilabiro na Incenerator na Placenta Pit vinawia mikono na mabomba ya maji 4 Zahanati ya Churazo kwa gharama ya Tshs. 31,424,580/=, Wodi ya Wazazi Nyamtukuza kwa gharama ya Tshs. 65,110,630/=, Vyoo matundu (8)Shule ya Msingi Keza kwa gharama ya Tshs.52,697,534/=, Vyoo Matundu (8) Shule ya Msingi Nyanzige kwa gharama ya Tshs.52,747,534 na Mabomba ya maji (10) shule ya msingi Nyanzige kwa gharama ya Tshs.19,969,723/=.
Bi.Bertha ameushukuru uongozi wa Wilaya na Halmashauri kwa ushirikiano walioutoa kwani mara baada ya miradi kukamilika ilianza kutumika kusaidia jamii.
Aidha Bi. Bertha ameeleza mwaka huu 2023 Shirika la World Vision limekabidhi Vifaa tiba kwa Mganga Mkuu Vyenye thamani ya Milioni Tisini na mbili na samani (funiture) zenye thamani ya Milioni Ishirini na tatu kwa ajili ya kutumika katika zahanati (4).
Shirika la World Vision pia limetoa Bima za Afya za CHF kwa familia 1000 kwa kanda ya Kasanda na Nyaronga na Bima hizo zinafanya kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa Kutoa kibali kwa mashirika kufanya kazi Tanzania na amelipongeza Shirika la World Vision kwa kujenga miradi yenye viwango na kwa gharama kubwa na kuwasihi kuendelea kusaidia na maeneo mengine yenye changamoto kwani bado yapo lakini pia Serikali ya Tanzania inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu na huduma kwa kuleta watumishi katika Sekta za Afya na Elimu.
Kanali Mallasa amewataka Wananchi kutumia miundombinu hiyo kupata huduma bora na kuepuka kutumia tiba asilia bali wafike katika zahanati kupata huduma za uzazi na matibabu.
Vile vile amewasisitiza Wananchi na wanafunzi kutunza na kulinda miundombinu hiyo kwa kufanya usafi ili kuepuka magonjwa ya mlipuko na kutunza mazingira.
Katika hatua nyingine Bi. Isabella Mwakabonga Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Kakonko amelishukuru shirika la World Vision kwa kujenga vyoo katika shule zilizokuwa na changamoto ya matundu ya vyoo pia ameliomba shirika likipata nafasi lisaidie kujenga nyumba za watumishi.
Diwani wa Kata ya Nyamtukuza amelipongeza Shirika la World Vision kwa kujenga miradi hiyo na kuwasisitiza wananchi kuitunza na kuilinda moundombinu hiyo ili iwasaidie.
Paulina Renatus Mwananchi wa Kata ya Nyamtukuza ameeleza analipongeza Shirika la World Vision kwa kuwajengea wodi ya wazazi karibu na makazi yao kwani kabla ya hapo walikua wanapata huduma mbali, hivyo wamefurahi sana na amewaasa wanawake wenzake wanaojifungulia nyumbani na kwa waganga wa jadi waache tabia hiyo na wafike katika zahanati kujifungua kwani kwa sasa huduma zinapatikana bila shida.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa