Mafunzo ya uanzishwaji wa mfumo wa uthibiti ubora wa shule yanayolenga kushirikisha wadau katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza mashuleni na kurahisisha mawasiliano katika ngazi zote, yamefanyika katika ofisi za uthibiti ubora wa shule zilizopo kanyamfisi wilayani kakonko leo Alhamisi, tarehe 17 Aprili 2025.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, afisa uthibiti ubora wa shule, Wilaya ya Kakonko, Japhet Mbaga ameeleza kuwa Mfumo wa Uthibiti ubora wa Shule utakuwa ni chachu kwa Idara ya uthibiti ubora na wadau mbalimbali kwani utarahisha tathmini zinazofanyika shuleni.
Aidha ameongeza kuwa matumizi ya mfumo huo yataboresha utendaji kazi kwani utaondoa utaratibu wa kutumia karatasi wakati wa tathmini badala yake taarifa zote zitakuwa zinajazwa kwenye mfumo.
Mafunzo haya yamewahusisha viongozi wa halmashauri wakiwemo maafisa elimu sekondari na msingi, Maafisa Tehama pamoja na wathibiti ubora.
Hii ni awamu ya kwanza ya mafunzo ambapo awamu ya pili itafanyika baada ya sikukuu za pasaka ambapo itahusisha maafisa elimu kata (13), walimu wakuu (70), wakuu wa shule (25) na wenyeviti wa kamati za ndani za uthibiti ubora wa shule.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa