Tsh.2.1 bilioni zinatarajiwa kutumika kujenga stendi ya kisasa katika kipindi cha siku 365 kuanzia Mei 30, 2019 na kuleta mabadiliko chanya kiuchumi kwa wakazi wa Kakonko na Halmashauri kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Masumbuko Stephano Magangāhila katika hafla ya kusaini mkataba iliyofanyika hivi karibuni kwa kampuni ya M/S SUGWA CONTRACTORS ENTERPRISES LTD JV CHIGANDA CONSTRUCTION COMPANY LTD SLP 121 CHATO- GEITA iliyoshinda zabuni hiyo.
Kampuni hiyo inatarajiwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa stendi ya kisasa kwa Tsh.2,146,996,675.79 ambapo kutakuwa na majengo ya utawala ya kisasa, maduka yasiyopungua 20 ya kufanyia biashara, eneo la maegesho magari makubwa, madogo, pikipiki na bajaji pamoja na kutengeneza eneo la stendi vizuri na kuhifadhi eneo linguine kwa matumizi ya baadaye.
Aidha kampuni ya M/S OGM CONSULTANTS YA DAR ES SAALAM imeshinda zabuni ya kazi ya ushauri kwa Tsh.128,147,000 katika kusimamia na kutoa ushauri katika ujenzi wa stendi mpya.
Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Maganga ameeleza kuwa wananchi wanatarajia mradi huo utaisha kwa wakati na kuleta mabadiliko makubwa kwao ya kiuchumi kwani utapanua wigo wa kibiashara na kutoa fursa za ajira kwa wakazi wa Kakonko hivyo kuinua kipato cha Wilaya na mwananchi mmoja mmoja.
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesisitiza mkandarasi kutekeleza mradi kwa ufanisi na kukamilisha kwa wakati huku akimsisitiza Mkurugenzi mtendaji kuchukua hatua ikiwemo kuvunja mkataba iwapo kampuni iliyoshinda zabuni itaonekana kushindwa kutekeleza kazi hiyo kwa wakati kwani fedha zipo.
Hata hivyo tayari kampuni ya Sugwa imeanza kazi ya kusafisha eneo na kuzungushia uzio ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa stendi ya kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
HatimilikiĀ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa