Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Jimbo la Buyungu Ndaki Stephano Mhuli leo Jumanne Oktoba 1, 2024 amekutana na Viongozi wa kamati ya maridhiano ya dini mbalimbali na viongozi wa Vyama vya siasa na kuwaomba kuwahamasisha waumini na wafuasi wa vyama kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mkazi Oktoba 11-20, 2024 ili kuweza kupiga kura na kuchagua Viongozi wao ifikapo Novemba, 27, 2024.
Akizungumza na Viongozi wa dini, Msimamizi wa Uchaguzi amewaomba viongozi hao kuendelea kuhamasisha na kuhubiri amani katika maeneo ya ibada ili wananchi washiriki uchaguzi kwa amani na utulivu wakati utakapofika.
Aidha msimamizi amewaomba viongozi wa siasa kufanya siasa za kistaarabu wakati wa kampeni utakapowadia ili kutunza amani iliyopo.
Kamati ya maridhiano ya dini mbalimbali ilikutana saa 3 asubuhi leo Jumanne katika Ukumbi wa Gombe uliopo Wilayani Kakonko na Msimamizi wa uchaguzi na wajumbe wa Timu ya Uratibu wakati Viongozi wa Vyama vya siasa walikutana na msimamizi wa Uchaguzi na timu yale saa 7 mchana katika Ukumbi huo wa Gombe, wote wakipitishwa katika ratiba ya Uchaguzi na kanuni zake na kuelezwa idadi ya vituo vya kujiandikisha na kupiga kura kuwa ni 358 ambapo kati ya hivyo 69 vitakuwa katika majengo yasiyo ya umma hivyo kujengewa mahema.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa