Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa, amewataka wataalam wanaosimamia na kuratibu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya wilaya ya Kakonko kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo kwa kiwango kilichoainishwa kwenye mikataba.
Rai hiyo imetolewa Disemba 18 2024, na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col. Evance Mallasa wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.
Aidha amewataka wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi ili kufikia Januari 13, 2025 miradi yote iwe imekamilika kwa kuzingatia vipimo na michoro ya majengo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Bw.Ndaki Stephano Mhuli, amewaelekeza wahandisi wa ujenzi kuendelea kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo kwa lengo la kushughulikia changamoto pamoja na kutoa taarifa ya kila kinachoendelea wakati wote wanapokuwa katika maeneo ya miradi.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kijiji cha Bukirilo, ujenzi wa madarasa manne (4) na matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Kiga, ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kijiji Luhuru pamoja na ujenzi wa madarasa ya awali katika shule ya msingi Itumbiko.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa