Wakazi wa Kijiji cha Nyamtukuza Kata ya Nyamtukuza kilichopo tarafa ya Nyaronga wameeleza kuwa kukosekana kwa soko kumewasababishia adha mbalimbali ikiwemo kunyeshewa na mvua wanapokuwa wakipata mahitaji yao eneo la soko.
Eliana Thobias mkazi wa Kijiji cha Nyamtukuza ameeleza shida kubwa waliyokuwa nayo ni kukosekana kwa soko.
Naye Apolonia Sebastian Mjumbe wa kamati tendaji ameeleza kuwa walikuwa wanahainga mhali pa kuuzia mvua ikinyesha na kueleza kuwa majiyalikuwa yanawafikia mahali wanapouzia.
Bwana Josephat Raphael Kazingo, Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Kijiji cha Nyamtukuza ameeleza kuwa ukamilishaji wa soko utasaidia kuepuka akina mama kunyeshewa bidhaa zao ikiwemo matunda ambayo yalikuwa yananyeshewa na kuingia uchafu hivyo kuomba mazingira ya soko kuboreshwa.
Akitoa mrejesho katika soko la Nyamtukuza mwanzoni mwa mwezi Mei, 2023 kuhusu ujenzi wa soko la Nyamtukuza diwani wa Kata ya Nyamtukuza Mhe.Abdallah Rajabu Maghembe ameeleza kuwa Mhe.Mbunge Aloyce Kamamba kupitia mfuko wa Jimbo amechangia milioni 18 kujenga soko la Kijiji cha Nyamtukuza ili kuondoa kilio cha muda mrefu cha Wananchi kujengewa soko.
“Simenti imeingia mifuko 250, mabati 200 yameingia, tuna kazi ya kupasua mbao tutaenda kuomba kibali, milioni 4 na laki 3 ipo kwenye akaunti, alieleza Mhe.Abdallah Magembe.
Akiwakilisha wajumbe wa mfuko wa jimbo katibu wa mbunge Jimbo la Buyungu Eliud Jackson amewaeleza wananchi kuwa mfuko wa Jimbo umechangia mfiko 250 ya simenti na mabati 200 ili kukamilisha ujenzi wa soko la Kijiji cha Nyamtukuza na kuondoa adha mbalimbali waliyokuwa wana kumbana nayo wananchi ikiwemo kunyeshewa na mvua sokoni hapo.
Katibu ameeleza kuwa mbunge ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa Jimbo kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji amnbaye ni katibu pamoja na wajumbe wa kamati wanatarajia viongozi wa Kijiji kushirikiana kusimamia ujenzi wa soko ili ujenzi ukamilike kufikia mwezi Juni, 2023 na kamati itatembelea eneo hilo kujiridhisha iwapo ujenzi umekamilika.
Wajumbe wa mfuko wa jimbo wamekabidhi vifaa mbalimbali katika kata ya Nyamtukuza, Nyabibuye na Gwarama vyenye thamani ya Tshs.77,136,000 kukamilisha miradi iliyofadhiliwa na mfuko wa Jimbo ambapo Kijiji cha Nyamtukuza ndio kimepewa fedha nyingi zaidi Tshs.18,000,000 ukilinganisha na kata ya Nyabibuye na Gwarama.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa