Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa ameahidi kuchukua hatua kwa wakulima wanaochanganya zao la pamba na mazao mengine na kuagiza apatiwe orodha ya watu waliochanganya mazao.
Aidha ameagiza watu waliochukua viwatilifu na hawana mashamba warudishe.
Col.Mallasa ameyasema hayo katika semina iliyoendeshwa na Balozi wa pamba Tanzania Aggrey Mwanri Machi 27, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Balozi Mwanri alikutana na na waheshimiwa Madiwani, Mwenyekiti wa CCM (W), Viongozi wa AMCOS, Watendaji wa Kata na Vijiji na wadau mbalimbali walioalikwa ambapo alilaani watu wanaochukua viwatilifu bila kutumia na wale wasiomwagilia sumu ya wadudu kwa usahihi na kusema kuwa dawa ni feki.
Waheshimiwa madiwani, watendaji wa kata na Vijiji na wadau wengine wameahidi kutoa elimu waliyoipata kwa wakulima ili kuleta tija katika ulimaji wa pamba katika Wilaya ya Kakonko.
Balozi Mwanri alianza ziara ya kutembelea wakulima siku ya Jumamosi tarehe 25 Machi na kuhitimisha Jumatatu tarehe 27, Machi 2023.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa