Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa amewahimiza wakulima Wilayani Kakonko kuongeza thamani ya mazao.
Ameyasema hayo katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane ambayo yamefanyika Agosti 05,2023, katika kijiji cha Nyakiyobe Kata ya Gwarama.
Kanali Mallasa amewasisitiza Wakulima kuepuka kulima mazao kwa kutumia njia za kitamaduni bali wabadilike na kuanza kutumia njia za kisasa ambapo kuna vifaa vya kisasa ambavyo vitawasaidia katika uzalishaji na uchakataji wa mazao ya Alizeti,Mahindi, Mihongo pamoja na Shughuli za umwagiliaji kwa muda mfupi.
Aidha Kanali Mallasa amewataka wataalam wa kilimo kufika katika mashamba ya wananchi kuwasaidia Wakulima kwa kuwaelimisha njia bora za kutumia katika kilimo.
Vile vile amewahakikishia wakulima kuwa ameshafanya Mawasiliano na Wizara ya Kilimo wameahidi kuleta mbolea kwa wakati na mbolea hizo zitawafikia wakulima katika maeneo yao.
Mhe. Aloyce Kamamba Mbunge wa Jimbo la Buyungu amewataka wakulima na wafugaji kuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali ikiwemo zao la Pamba, Alizeti, Migomba na mazao mengine.
Kwa upande wake Fidel Nderego Diwani wa Kata ya Gwarama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko amewasisitiza Wananchi kuwekeza katika kilimo, ufugaji na Ujasiliamali.Vile vile amewataka wanachi kupiga vita uchomaji holela wa misitu kwakuwa hauna tija kwa uzalishaji wa kilimo na misitu.
Naye Saamoja Ndilaliha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kakonko amewahimiza wananchi kuzingatia kilimo kwani ndiyo uti wa mgongo.
Kauli Mbiu"Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula".
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa