Akifungua Mafunzo Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ambae pia ni Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya Dkt. Godfrey Kayombo ameelezea madhara yatokanayo na sumukuvu ambapo amesema kuwa lengo ni kuwajengea uwezo na uelewa walimu ili waweze kuwa na uelewa juu ya sumukuvu na namna bora ya kudhibiti sumukuvu katika kila hatua ya utunzaji na uandaaji wa chakula shuleni.
Mafunzo haya yamefanyika tarehe 06.01.2025 na kuhudhuriwa na Maafisa elimu Msingi na Sekondari, Maafisa Ugani, Wakuu wa shule kutoka shule 22 za Sekondari na Walimu Wakuu kutoka shule 70 za msingi zilizopo wilayani.
Aidha mafunzo haya yalikua na dhima katika matumizi salama ya chakula na namna wanaweza kudhibiti sumukuvu wakati wa kuhifadhi nafaka kwani kuna mambo yakuzingatia wakati wa uandaaji wa nafaka kwa ajili ya chakula, hivyo wamesisitizwa kuzingatia matumizi sahihi ya uandaaji wa nafaka kwani sumukuvu zinakuwepo kwenye chakula.
Wakati akiendelea na mafunzo hayo ameeleza kuwa nafaka hususani mahindi na karanga viko kwenye hatari zaidi ya kushambuliwa na kuvu ambayo inazalisha sumukuvu.
Wakati akihitimisha mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza kuwa pamoja na kudhibiti sumukuvu wakati wa uandaaji wa chakula mashuleni wanapaswa kuzingatia matumizi ya Nishati safi.
Hata hivyo Halmashauri inaendelea na msisitizo wa kutumia nishati safi wakati wa uandaaji wa chakula shuleni kwa chakula ambacho kinaandaliwa kwa zaidi wa watu 100.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa