Walimu mbali mbali wa somo la hisabati na viongozi wa Elimu ngazi ya mkoa, wilaya na kata Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Wakishiriki Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini ili kuongeza mbinu mbali mbali za ufundishaji na ujifunzaji wa somo la hisabati kwa lengo la kuongeza ufaulu.
Mafunzo haya yamehusisha walimu 50 wa somo la Hisabati kwa shule za msingi kutoka kata mbali mbali hapa Wilayani Kakonko, na hii ni kwa sababu ya ufaulu mdogo ulioonekana katika somo la hesabu katika wilaya hiyo kimkoa na kitaifa. Hivyo Mafunzo haya yamelenga kuleta mbinu na dhana mbalimbali zitakazotumiwa na walimu hao katika kuongeza ufaulu wa somo hilo.
Walimu wameelekezwa kutumia mbinu mbali mbali kama vile kutumia mbinu shirikishi kufundishia na kujifunza somo la hisabati, pia washauriwa vitendo vingi vifanywe na wanafunzi ili kupima uelewa wao na ustadi wao, dhana zipitiwe kabla hazijapelekwa darasani kwa wanafunzi, pia walimu wazingatie uhitaji wa wanafunzi wanapokuwa darasani kama vile wanafunzi wenye mapungufu(disabilities), wanafunzi wapewe nafasi za kujadili, Kutumia mbinu ya Ninafanya, tunafanya, unafanya(I do, We do, You do.), Vilevile walimu wanapokuwa wanafundisha wajitahidi kupita kwa wanafunzi ili wajue wanafanya nini na wanaelewa vipi.
Walimu walioshiriki mafunzo wame wapongeza sana wadau wanaosimamia mafunzo haya kwani yamewajenga na wameahidi kuwasilisha vyema mafunzo hayo kwa walimu wenzao ambao hawakupata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya zamani ya wilaya ya Kakonko na yanafadhiliwa na shirika la Ukaid kupitia programme ya shule bora.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa