Walimu wa Shule za Awali na Msingi wametakiwa kuibua Hadithi za Mafanikio za mfano ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji ambazo zitaleta matokeo chanya kwa wanafunzi, katika Mwendelezo wa mafunzo ya Hadithi za Mafanikio za Kujifunza za mfano yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Kasanda Wilaya ya Kakonko Mkoani kigoma, siku ya Jumatatu tarehe 05 Desemba 2022.
Ameyasema hayo Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ualimu Bustani-Kondoa Ndugu Manoni Migabo alipokuwa akitoa Mafunzo kwa Walimu wa Shule za Awali na Msingi waliopo kazini pamoja na Wasimamizi wa Elimu ngazi ya kata zilizopo Kasanda na Kata ya Gwanumpu.
Aidha Walimu wanatakiwa kuandaa mpango kazi utakaowasaidia kuboresha ufaulu wa wanafunzi na kuleta Matokeo chanya.
Washiriki wameeleza Hadithi za Mafanikio za kujifunza za mfano ili waweze kufanikiwa kuzitumia na kuleta tija wanatakiwa kutumia mpango kazi ipasavyo.
Washiriki wameeleza ili kushiriki/kusambaza Hadithi za Mafanikio za kujifunza za mfano kwa watu wengine wanapaswa kutumia Mitandao ya kijamii, Mfumo wa kujifunza wa kimtandao (LMS) Learning Management System, Television, Radio, Machapisho, Vipeperushi pamoja na Majarida.
Kwaupande mwingine Manoni Migabo wakati akihitimisha Mafunzo amewahimiza Walimu wenye Hadithi za Mafanikio za kujifunza za mfano kujitokeza kwa wingi kwani watanufaika zaidi.
Mikoa inayotekeleza programu ya Shule bora Nchini Tanzania ni pamoja na Mkoa wa kigoma, Mara, Simiyu, Pwani, Singida, Katavi,Tanga, Dodoma na Rukwa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa