Wanafunzi wa kidato cha sita wanaojiandaa kufanya mitihani wamesisitizwa kutokujiingiza kwenye wizi wa mitihani, kutizamiana na mawazo ya udanganyifu bali wamtangalize Mungu na kufanya mitihani kwa kadiri walivyojifunza.
Akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya dini ya wanafunzi wa kidato cha sita wa kipentekoste (HUIMA) katika shule ya Sekondari Kakonko mwishoni mwa wiki Machi 10,2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndaki Stephano Mhuli ameeleza kuwa watu wanaoibia kwenye mitihani ni hasara kwa taifa kwani watapatikana wasiokuwa na uwezo wa kielimu hivyo kuwa tishio kwa usalama wa nchi.
“Lazima wanafunzi muwe waaminifu, mtangulize Mungu, msome kwa bidii na kuvuna mlichopanda ili Taifa lizidi kusonga mbele na kuinuka, ili waajiriwe watu wenye sifa nzuri wasiwepo vihiyo”, Alisema Mkurugenzi Ndaki,
“Tunasimamia kwa nguvu zetu zote kuhakikisha hakuna wizi ili tupate watu kwa sifa zao na uwezo wao, wafanye kazi wafikirie (critical thinkers), lazima wanafunzi wawe waaminifu ili wanapoajiriwa wafanye kazi”, aliongeza Mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Ndaki aliongeza kuwa wanafunzi wanaofaulu kwa kuibia mitihani wakiaajiriwa wanakuwa hawajitumi na hawana uwezo wa kuandaa mpango kazi badala yake wanasubiri kutumwa na bosi na wasipotumwa wanarudi nyumbani bila kufanya kazi hivyo kunakuwa hakuna uzalishaji wenye tija.
Mkurugenzi Ndaki aliendelea kusema kuwa, ‘Mtu hawezi kuishi nje ya maarifa aliyonayo hivyo mwanafunzi anavyosoma kwa bidii ndivyo anavofaulu kwani ndio uwekezaji alioufanya alieleza hakuna muujiza wa kufaulu bila kusoma.
Mkurugenzi Ndaki alimnukuu Mwalimu Julius Nyerere aliyetolea mfano mtu aliyeaminiwa na kupewa chakula na Kijiji chake ili kwenda Kijiji cha mbali kutafuta chakula lakini alipofika huko hakurudi alieleza kuwa huo ni usaliti ni sawa na mwanafunzi aliyeaminiwa na wazazi wake wakajinyima na kutoa fedha ili mtoto wao asome lakini mwanafunzi anapofika shuleni hasomi.
Tawi la HUIMA lilianza mwaka 2012 ambap hadi sasa lina wanachama 139 kati yao kidato cha 6 ni 32, kidato cha 5 ni 24, kidato cha 4 ni 18, kidato cha 3 ni 15, Kidato cha 2 ni 20 na kidato cha 1 ni 30.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa