Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya Msingi Itumbiko wamepokea msaada wa vifaa ikiwemo magodoro, neti pamoja na blanketi kwa ajili ya bweni lao kutoka shirika la Help age International wenye thamani ya Tshs.10,770,480 siku ya Ijumaa tarehe 25.03.2022.
Akitoa vifaa hivyo kwa niaba ya shirika la Help age International Bwana Abdul Issa ameeleza kuwa shirika limetoa Magodoro 80, blanketi 80 na Neti 80 kwa ajili ya bweni la watoto wenye mahitaji maalum.
“Kipekee tulipokea uhitaji wa vifaa kwa ajili ya malazi kwa ajili ya shule ya msingi Itumbiko na kama shirika la Help Age tuliamua kusaidia juhudi za Serikali kuendeleza elimu kwa kutoa magodoro 80 yenye thamani ya Tshs.6,102,000, Blanketi 80 zenye thamani ya Tshs.2,774,080 na neti 80 zenye thamani ya Tshs.1,894,080 jumla ya vitu vyote ambavyo tumevileta vina thamani ya Tshs. 10,770,480. Tunaamini kwa vitu hivi ambavyo tumevileta vitasaidia katika kufanya ujumuishwaji wa watu wenye mahitaji maalum katika kupata elimu wakiwa na wanafunzi wenzao watajisikia furaha na Amani wakiwa katika mazingira mazuri”. Alisema, Bwana Abdul, Mwakilishi wa Shirika la Help Age International.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Joseph Mutahaba ameshukuru kwa msaada uliotolewa na Shirika la Help Age International kwa msaada walioutoa na kueleza imekuwa msaada mkubwa. Ameongeza kuwa Shirika hilo hapo awali lilitoa msaada wa baskeli za walemavu 10 hivyo wanatambua mchango wao.
Mwalimu Berda Marko Koko anayewahudumia watoto wenye mahitaji maalum ameshukuru kwa msaada uliotolewa na kusisitiza wadau mbalimbali wasisite kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum.
Pili Sylivester Majaliwa mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu anayesoma darasa la nne ameshukuru wote waliojitolea kusaidia watoto wenye mahitaji maalum.
ambalo tayari limeezekwa na kufanyiwa usafi ndani yakibaki mapungufu kadhaa kukamilisha kabla ya kuanza kulitumia.
Halmashauri ilipokea fedha za UVIKO-19 zilizotolewa na Serikali Tshs.80,000,000 ambazo zimetumika na kuisha.
Ujenzi ulianza tarehe 01/11/2021 ambapo kazi zilizofanyika ni usafishaji wa eneo, ujenzi wa jengo na upakaji rangi kwa ndani. Wananchi wamechangia Tshs.635,000. Kiasi cha Tshs.79,998,650 kimetumika ambapo gharama za vifaa ni Tshs.65,798,650 na gharama za ufundi ni Tshs.14,200,000 na salio ni Tshs.1,350.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa