Wananchi wa Wilaya ya Kakonko wataanza kunufaika na huduma ya Afya ya dharura kufuatia kukamilika kwa jengo la dharura (EMD) lililojengwa katika hospitali ya Wilaya ya Kakonko iliopo Eneo la Itumbiko kata ya Kakonko mjini. Jengo hilo limejengwa kwa thamani ya Tshs.300,000,000 Milioni mia tatu na kukamilika mwezi huu wa Septemba, 2022.
Jengo hili litatoa huduma kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali watakoukuwa wanakuja katika Hospitali ya Wilaya ya Kakonko kwa dharura hivyo kupata huduma katika jengo hilo kwanza kabla ya kupelekwa maeneo mengine ya huduma.
Ujenzi wa majengo 8 umekamilika katika hospitali ya Wilaya ya Kakonko ukihusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD), jengo la Mionzi, Maabara, Wodi ya wanawake, Jengo la kufulia, Jengo la dawa, Jengo la Utawala na Nyumba za Watumishi (3 in 1).
Ujenzi wa majengo hayo 8 umegharimu Tshs.2,190,000,000 (bilioni mbili laki moja na elfu tisini)
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa