Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa ametoa rai kwa wananchi wa Wilaya ya Kakonko kuanza kuitumia Mahakama ya Wilaya kutatua migogoro ya mashauri ya kisheria kwa njia ya usuluhishi.
Amesema hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Sheria yaliyofanyika katika viwanja vya majengo mapya ya Mahakama ya Wilaya ya Kakonko eneo la Kanyamfisi Mwanzoni mwa mwezi Februari, 2023 na kuwasisitiza Wananchi pale ambapo hakuna hitaji la msingi kutatua migogoro kwa njia ya Mahakama na Sheria ni vizuri wakatumia njia ya usuluhishi kwani inatumia muda mfupi kufikia maamuzi.
Ameendelea kusema njia ya usuluhishi ni utaratibu wa kumaliza mgogoro kwa njia ya mapatano kutoka kwenye pande mbili zenye mgogoro kwa kushirikisha mtu au pande tatu na kuna wakati vifungu vya sheria havitimiki kwa hiyo hii ni njia ya kutatua migogoro kwa njia ya makubaliano.
Aidha katika njia ya usuluhishi anayehusika kusuluhisha huwa hana amri ya maazimio ya shauri au kesi hiyo, kwani kuna kesi nyingi za mashauri zinaweza kusuluhishwa kwa njia ya usuluhishi mfano kesi za madai, ndoa na migogoro ya ardhi kwani njia hii ni nzuri na hakuna mshindi wa kesi au mashauri hayo bali ni makubaliano ya kumaliza changamoto hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa