• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe |
Kakonko District Council
Kakonko District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Mawasiliano
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Usafishaji Na Mazingira
        • Elimu Msingi
        • Elimu ya Sekondari
        • Afya na Ustawi wa Jamii
        • Maji
        • Maendeleo ya Jamii
        • Utumishi na Utawala
        • Fedha na Biashara
        • Maliasili, Ardhi na Mazingira
        • Kilimo cha Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Ujenzi na Zimamoto
      • Vitengo
        • Ugavi na Manunuzi
        • Tehama na Habari
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ufugaji Nyuki
        • Uchaguzi
        • Sheria
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Livestock
    • Fisheries
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Usimamizi
      • Elimu Afya na Maji
      • Huduma za Kiuchumi Ujenzi na Mazingira
      • Udhibiti wa UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao
        • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayo tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WAONYWA KUACHA KUFUMBIA MACHO VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA.

Imetumwa: March 3rd, 2023

Halmashauri imewasisitiza Wananchi kutofumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapotokea katika jamii badala yake watoe taarifa kwa Viongozi ngazi ya Kata, Dawati la jinsia na kwenye Kamati zilizoundwa kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya ukatili wa   kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika mwanzoni wa wiki hii siku ya Jumanne katika Kata ya Kasanda Wilayani Kakonko kwa Wananchi pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kasanda, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya Mustapha Mtungwe amesema kuwa  utoaji Elimu ni moja ya jitihada za kutokomeza ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto.

Bwana Mustapha ameeleza kuwa kumekuwa na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyofanyika katika ngazi ya kaya na shuleni wakati huohuo ukatili unaondelea kwa sasa ni ukatili dhidi ya watoto kwa watoto wenyewe hivyo amewasisitiza wazazi kuwafuatilia watoto wao kwa ukaribu wasifanyiwe vitendo hivyo na kuwaomba kuwa makini kwani kumekuwa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotumiwa kutoa hamasa juu ya suala la ukatili wa kijinsia lakini wakati huohuo wanafundisha masuala yaliyo kinyume na maadili ya Watanzania.

 

 

 

“Tuendelee kushirikiana wote kwa pamoja kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsi dhidi ya wanawake na watoto katika jamii zetu”, Alisema Afisa maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kakonko Bwana Mustapha Mtungwe.

Naye Afisa maendeleo ya jamii  Bi. Safia Mjubeli amewaomba wananchi wasiogope kutoa taarifa pindi watakapongundua kuna mtu katika jamii anafanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwasisitiza waendelee kushirikiana katika kuhamasishana na kutoa elimu kwa jamii kwani wengi wao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo na kukaa kimya hivyo tatizo kuendelea kuwa kubwa katika jamii inayowazunguka.

“Sisi  Maafisa Maendeleo ya Jamii tunahamasisha Jamii kuhakikisha vitendo hivi vinaisha katika jamii zetu hivyo tushikane mikono kwa pamoja tupinge ukatili wa kijinsia katika jamii”, Alisema Bi.Safia  Mjubeli.

 Mtendaji wa Kata ya Kasanda, Alexander Mwalemba amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanatokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii kwani vitendo hivyo vimekuwa vikitokea lakini kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamejitahidi kuvizuia na wameandaa programu itakayosaidia kutoa Elimu kwa kamati zilizoundwa kwa ajili ya kushughulikia suala la ukatili wa kijinsia na kutambua majukumu yao kuhakikisha vitendo vinavyotokea katika jamii vinaripotiwa ofisi ya kata.

Naye Tabu Peter Mkazi wa kata ya Kasanda amesema kuwa wanawake wengi wanafanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo amewaomba viongozi kuendelea kutoa elimu wasiishie ngazi ya kata tu na badala yake wafike kutoa elimu ngazi ya kitongoji kwani itasaidia zaidi kutokomeza vitendo hivyo. Vilevile amewashauri wanawake wanaofanyiwa vitendo hivyo wasikae kimya watoe taarifa sehemu husika ili wapate msaada.

Kuelekea siku ya Wanawake duniani Divisheni ya Maendeleo ya Jamii imefanya mikutano ya hadhara katika Kata mbalimbali pamoja na shule za Sekondari na Msingi kwa lengo la utoaji Elimu juu ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na Watoto.

Divisheni ya Maendeleo ya Jamii imetembelea Kata ya Kasanda, Kiziguzigu, Kakonko na Kata ya Kanyonza na kufika katika shule mbalimbali ikiwemo shule ya Sekondari Kasanda, Buyungu na Kakonko  pamoja na shule ya msingi Ilabilo na Kihogazi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani mwaka 2023 inasema, “Ubunifu na mabadiliko ya Teknolojia, chachu katika kuleta usawa wa kijinsia”.

Siku ya Wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka kuanzia Machi 1 na kufikia kilele Machi 8 ambapo mwaka huu Kiwilaya yataadhimishwa Machi 6 katika Kata ya Kasanda Wilayani Kakonko ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya Kanali Evance Mallasa.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - WAKUSANYA MAPATO January 30, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. June 18, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA YA WAOMBAJI NAFASI YA UKUSANYAJI MAPATO WALIOITWA KWENYE USAILI January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI WA VITENDO - WAOMBAJI KAZI YA DEREVA II November 17, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PSSSF YARAISISHA HUDUMA KWA WASTAAFU KUPITIA MIFUMO YA KIDIJITALI.

    May 29, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KAKONKO ROBO YA TATU 2024/2025 LAWEKA MKAZO MAENDELEO, UWAJIBIKAJI NA USHIRIKIANO WA PAMOJA.

    May 21, 2025
  • HALMASHAURI KUU YA WILAYA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) YA KAKONKO YAPONGEZA UWAJIBIKAJI NA UTENDAJI KAZI MZURI WA KAZI KWA VIONGOZI.

    May 14, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KAKONKO

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkurugenzi afafanua mikakati ya kuendeleza zao la parachichi ikiwemo kugawa mashamba kwa wananchi.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Watendaji
  • Ukaguzi wa Miradi Kakonko
  • Lori jipya la Halmashauri laongeza kasi ya utekelezaji Miradi ikiwemo mradi wa Ufyatuaji tofali
  • TASAF kuibua ajira Kakonko
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko - FACEBOOK account
  • Habari motomoto za magazeti kila siku
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO- INSTAGRAM ACCOUNT
  • WANAFUNZI WILAYA YA KAKONKO WALIOPANGIWA SHULE KIDATO CHA KWANZA
  • MATOKEO YA WANAFUNZI WA DARASA LA NNE WILAYA YA KAKONKO 2022

Viunganishi linganifu

  • Poralg
  • Public Service Management and Good governance
  • Necta
  • Tanzania portal
  • Kigoma Region Website
  • Tangazo la nafasi za kazi
  • Matokeo kidato cha nne 2018/2019 haya hapa
  • Balozi wa Norway akabidhi vifaa vya mifugo kakonko
  • Bunge la Tanzania
  • kakonko tv
  • Mapinduzi sekta ya elimu Kakonko
  • halmashauri ya wilaya ya kakonko - habari na mawasiliano
  • MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA 2 MWAKA 2022

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 3

    Simu: +255(028) 2988881

    Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881

    Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz

Mawasiliano

   

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma
    • Kanusho

Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa