Kampuni ya UNICORN HYGIENE TANZANIA COMPANY LIMITED imegawa boxi 18 za taulo za kike (pedi) kwa Wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Wasichana Kakonko ikiwa ni kurudisha kwa jamii mchango kwa kushirikiana na kampuni ya SINOTEC, TRACTEBEL, KFW na TANESCO.
Zoezi la ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi hao limefanyika mwishoni mwa wiki Juni 10, 2023 katika shule ya Sekondari ya Wasichana Kakonko yenye idadi ya wanafunzi 186.
Lengo la kutoa taulo za kike ni kuwasaidia Wanafunzi wa kike ambao wengi hawana uwezo wa kununua taulo hizo hasa wakati wanapozihitaji.
Akizunguzumzia suala hilo Meneja masoko wa kampuni ya UNICORN Goodlucky Calleb ameongeza kuwa utoaji wa taulo za kike utasaidia kuepuka utoro kwa Wanafunzi wa kike hasa wanapokuwa katika kipindi cha hedhi na kukosa taulo za kike hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao.
Kaimu Afisa Elimu Sekondari, Claudius Nzabayanga ameshukuru kampuni ya UNICORN na wadau wengine kwa kuchangia taulo za kike na kuendelea kuwaomba wadau hao kusaidia shule nyingine za Sekondari na msingi.
Akishukuru kwa niaba ya Wanafunzi wengine, Neema Francis John, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Wasichana ameeleza kuwa amefurahi kwa kupatiwa taulo za kike na kuomba wadau waendelee kuwasaidia vifaa vingine vinavyotakiwa kwa wanafunzi wa kike wawapo shuleni.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa