Kuelekea maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani tarehe 12 Mei, 2024 Shirika la TADEYO (Tanzania Development Youth Organization) kutoka Wilayani Kakonko kwa kushirikiana na Salama Foundation wamefanya mafunzo Siku ya Ijumaa Mei 10, 2024 kwa wauguzi na wakunga kuhusu akina mama wadogo yaani wanawake wanaopata mimba katika umri mdogo.
George Ngasa, Mratibu wa huduma za Afya ya uzazi na mtoto Wilaya ameeleza kuwa wamekuwa na mafunzo kuhusu wazazi vijana/wadogo kuanzia miaka 14-24 yakiwalenga watoa huduma za afya ya uzazi kutoka kliniki ya baba, mama na mtoto, wodi za wazazi pamoja na matabibu kutoka kituo cha Afya ya Kakonko na hospitali ya Wilaya.
Lengo la mafunzo hayo ni kuboresha huduma kwa wamama wadogo na kuwahudumia katika hali ya utu ili wajisikie vizuri badala ya kusikia kuhukumiwa.
Mratibu ameeleza changamoto kubwa ni upungufu wa watoa huduma katika maeneo ya kazi hivyo watoa huduma kufanya kazi nyingi na kuomba wadau kuongeza watoa huduma wenye ujuzi badala ya kujikita kutoa msaada wa wahuduma wa afya ngazi ya jamii.
Uwezo Ibrahim, muuguzi mfawidhi hospitali ya wilaya ya Kakonko ameeleza kuwa amejifunza kuwa wa mama wadogo wanastahili kupata huduma za afya ya uzazi hususani kipengele cha uzazi wa mpango bila ya ubaguzi.
Odes Sylivester Kiicha mtoa huduma kituo cha afya Kakonko ameeleza kuwa amjifunza mambo mengi ikiwemo uzazi salama kwa wamama wadogo ameongeza kuwa wazazi wengi hawapendi suala la uzazi salama kwa Vijana wadogo wanaopata mimba hivyo elimu inatakiwa kuendelea kutoalewa kwa jamii.
Stephen Bikoko Mkurugenzi wa taasisi ya TADEYO, ameeleza kuwa wameandaa mafunzo hayo kwa lengo la kuwajengea uwezo manesi na wauguzi ili kuwahudumia vizuri akina mama vijana. Ameeleza malengo ya taasisi ni kuhakikisha watoto wa kike wanafikia ndoto zake na jamii kubadilika ili kuleta matokeo chanya.
Jekoba Omary Dioff, mwakilishi wa Taasisi ya Salama Foundation ameeleza kuwa wameshirikiana na shirika la TADEYO ili kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa akina mama waliopata mimba katika umri mdogo. Ameeleza kuwa Kakonko kuna kiwango kikubwa cha idadi ya mabinti waliopata mimba katika umri mdogo hivyo Wilaya inatakiwa kutazamwa kwa jicho la tatu kwani mabinti wanaolewa katika umri mdogo.
Aidha changamoto hiyo ya kupata mimba katika umri mdogo insababishwa na watu wazima na mabinti wenyewe kukubali kujiingiza mkatika masuala ya ngono hivyo kutoa rai kwa jamii kutoa ushirikiano na kuahidi kutafuta wadau zaidi ili kuongeza watoa huduma.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa