Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa amewataka Wasimamizi wa Miradi kusimamia miradi kwa weledi kwa kufuata kanuni na sheria ili kuepuka adha ambazo zinaweza sababishwa na usimamizi hafifu wa miradi.
Alisema hayo katika Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani la robo ya tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2023 katika mwaka wa fedha 2022/2023 lililofanyika Aprili 28, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa kutoka Serikali kuu alieleza tayari Wilaya ya Kakonko imepokea Fedha za mradi wa BOOST Tshs. 1,457,800,000/= (Bilioni Moja Milioni Mia nne na Hamsini na Saba na Laki nane tu) za ujenzi wa miundombinu ya Shule za Msingi.
Alisema fedha hizo zinatarajia kujenga Shule Mbili Mpya za Msingi katika kata mbili (2) ambapo Shule moja itajengwa katika Kata ya Kasanda kijiji cha Kazilamihunda na Shule ya pili itajengwa katika kata ya Nyamtukuza kijiji cha Nyamtukuza. Aidha kutakuwa na ujenzi wa Vyumba (22) vya Madarasa, Nyumba moja ya Mwalimu na ujenzi wa Matundu (15) ya vyoo katika Shule nane (8) zilizo ndani ya Wilaya ya Kakonko.
Aidha Kanali Mallasa alieleza miradi ya maendeleo iwe ya mfano mzuri nasiyo mifano mibaya katika Halmashauri yetu ya kakonko.
“Nielekeze miradi ya BOOST isiwe na dosari za kitaalamu wala za kiutawala, nielekeze “task force” inayoundwa na wajumbe wa kamati ya usalama kuanza kazi mara moja itembelee miradi yote na ilete taarifa ya kina ili tuchukue hatua muafaka kwa wakati muafaka”. Alisema Kanali Mallasa
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa