Wataalamu wa Afya wemetoa Elimu kwa wananchi wa Kata ya Kanyonza na kuwasisitiza wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na kuzingatia matumizi ya vyoo bora kwani itawasaidia kulinda vyanzo vya maji na kujiepusha na mlipuko wa magonjwa mbalimbali.
Hayo yamesemwa na wataalamu wa afya walipokuwa wakitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Kanyonza iliyopo Wilayani Kakonko Mei 11, 2023 ambapo kupitia elimu hiyo jamii imejifunza namna ya uchafushaji na kusisitizwa kuendelea kuzingatia matumizi ya vyoo bora.
Joshua Joseph, Afisa Afya na Mazingira amesema kuwa lengo la utoaji elimu kwa jamii ni kuhamasisha wananchi na kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uelewa juu ya matumizi sahihi ya vyoo na utunzaji wa mazingira pia kuondoa dhana ya watu kuendelea kujisaidia nje ili kuisaidia jamii kutunza mazingira pia kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Ndaki Stephano Mhuli amewaomba wananchi kuzingatia elimu waliopewa na wataalamu wa afya pia kuhakikisha wanakuwa na matumizi sahihi ya vyoo hivyo kutojisaidia ovyo na badala yake kutumia vyoo kwani kujisaidia ovyo inaweza kuleta madhara ikiwemo mlipuko wa magonjwa mbalimbali hivyo wajitahidi kutunza vyanzo vya maji na kuzingatia matumizi bora ya vyoo.
Naye Diwani wa Kata ya Kanyonza, Mheshimiwa Alfred Elias amewashukuru wataalamu wa Afya kwa kufika kutoa Elimu kwa wananchi juu ya usafi wa mazingira na matumizi sahihi ya vyoo nakuwaomba wananchi kuzingatia elimu hiyo kwani Wananchi wengi wa kata hiyo hawana vyoo hivyo wajitaidi kuzingatia elimu, ameendelea kusema kama kiongozi ataendelea kuwahamasisha wananchi ili waweze kujenga vyoo na kuvitumia ipasavyo.
Mtendaji wa Kata ya Kanyonza, Donald Lukomanya amewasisitiza wananchi kujenga vyoo kwani wasipojenga na kuzingatia taratibu zote za afya ili waweze kuepuka magonjwa ya mlipuko, aidha amesema kama kata wamejipanga kuendelea kuhamasisha kwakushirikiana na wataalamu wa afya ili wananchi waweze kujenga vyoo ameendelea kusema hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kutozwa faini kwa wale watakaobainika hawana choo.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa