Watanzania wametakiwa kudumisha Amani, upendo na mshikamano wa kitaifa kama njia mojawapo ya kujiletea Maendeleo.
Wito huo umetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mzava wakati akikimbiza mwenye Wilayani Kakonko, leo Jumamosi Septemba 21, 2024.
Akipokea mwenge huo mkuu WA wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa amesema mwenge utaweka mawe ya Msingi, utatembelea, utakagu miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 2,339,638.41, huku Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri, Ndaki Stephano Mhuli akieleza mikakati mbalimbali aliyonayo katika kuhakikisha Wananchi wananufaika na miradi ya maendeleo inayoletwa na serikali katika halmashauri hiyo.
Baadhi ya wananchi Wilayani Kakonko wameipongeza serikali kwa kutambua kutoa fedha ambazo zimesaidia kukamilisha miradi mbalimbali iliyopo kwenye maeneo Yao ikiwemo ujenzi wa hospitali ya Wilaya, shule za msingi na Sekondari, Huduma ya Maji safi na Salama na miundo mbinu ya Barabara.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Kakonko umekimbizwa umbali wa kilomita 136 umeweka mawe ya Msingi, umetembelea na kukagua miradi 9 yenye zaidi ya shilingi bilioni 2.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa