Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa amawasisitiza Watumishi wa Wilaya ya Kakonko, Wakuu wa Taasisi za Serikali na zile zinazojitegemea, wadau na Wananchi kwa ujumla kushiriki katika Michezo kila siku ya Jumamosi asubuhi kwani michezo huimarisha Afya na ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita.
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya Mwenge katika kikao kilichofanyika leo Jumanne Julai 18, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri amesema kuwa suala la michezo sio kwa watumishi tu bali ni kwa watu wote hivyo kuwasisitiza Wajumbe na Viongozi wa makundi kuendelea kuhamasishana ili watu wote washiriki michezo ambayo inafanyika kila jumamosi kutokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Ndaki Stephano Mhuli ametoa rai kwa Watumishi wote kujitokeza katika michezo kwani mazoezi ni lazima kwa wote kiafya na kuongeza kuwa mazoezi yatafanyika ya kukimbia pamoja na mazoezi ya viungo uwanjani.
Mkurugenzi Ndaki ametoa maelekezo kwa Afisa michezo kuanzisha mechi kwa makundi mbalimbali wakiwemo watumishi wa Halmashauri na wale wasio watumishi wa Halmashauri na kueleza wataalam wa mazoezi ‘aerobic’ watasimamia michezo hiyo.
Akihitimisha hilo Mkurugenzi Mtendaji ametoa taarifa kuwa maboresho yatafanyika katika michezo ikiwemo ununuzi wa vifaa vya michezo kama jezi, mipira pamoja na basi la kubeba wana michezo kwa kuhusisha makundi mablimbali.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa