Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Michael Faraay amewahimiza Watumishi Wapya kuzingatia na kuyaishi yale ambayo watajifunza pia kuwa na mpango kazi utakao wasaidia kuendeleza majukumu yao pale watakapo kuwa katika vituo vyao vya kazi.
Alisema hayo mwisho mwa wiki hii wakati akifungua Mafunzo elekezi ya siku mbili Disemba 15 -16, 2022, kwa Watumishi wapya kutoka idara ya Afya, Elimu, na Utawala ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.
Kwaupande wake Afisa Utumishi Wilfred Ntagaye amesema kuwa lengo kubwa la Mafunzo ni kuwajengea uwezo Watumishi Wapya kufanya kazi katika misingi ya maadili ya utumishi wa umma kwani Mafunzo hayo yatawasaidia Watumishi ambao ndio watoa huduma kwa Wananchi na kutambua viashiria mbalimbali vinavyoweza kusababisha hatari katika utendaji kazi wao.
Radisilaus Ibrahim Kamanda Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Kakonko amewataka Watumishi Wapya kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani lengo la Serikali ni kuja kuwatumikia Wananchi wa Wilaya ya Kakonko na kuhakikisha kila Mwananchi anapata maendeleo kwa haraka kwa kuzingatia Huduma zinazotolewa kwa haki na usawa bila kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Aidha katibu wa Afya Kakonko Gwamaka Edison amewasisitiza Watumishi Wapya kuutumia umoja wao kama chombo cha kuwaunganisha na kushikamana katika matukio ya kikazi na kijamii.
Naye Afisa maliasili Wilaya ya Kakonko Bosco Huruma amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamia vyanzo vya maji na kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya utunzaji wa Mazingira kwani wao ndio wenye dhamana ya kusimamia Mazingira kikamilifu hivyo amewaomba kutunga Sheria ndogo ndogo ili kuthibiti majanga ya moto kwa kuunda Kamati ambazo zitasaidia kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya madhara ya uchomaji wa moto.
Kwaupande wake Afidhi Ramadhani Mtendaji wa Kata ya Katanga ambae ni mmoja wa Watumishi Wapya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko amesema kuwa kupitia mafunzo hayo wamejifunza mambo mengi hivyo ufanisi wao wa kazi utaenda kuongezeka katika utendaji kazi, vilevile wameahidi kwenda kufanya kazi ambayo itakuwa na tija kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Serikali.
‘’Tutaendelea kuwa wabunifu kwa kutumia Elimu rasimi na isiyo kuwa rasimi kuhakikisha tunafanya kazi kwa makini na kuleta tija katika kazi zetu lengo kubwa ni kuwasaidia Wananchi wa Wilaya ya Kakonko’’ Amesema Afidhi Ramadhani.
Eliwaza Petro Mwalimu wa Sekondari Buyungu ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kwa kuaandaa mafunzo hayo ambayo yatawajenga katika utendaji kazi kwa kuzingatia misingi ya maadili ya kiutumishi pia amewapongeza wakufunzi kwa kutoa mafunzo hayo kwani hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza na mafunzo yameisha salama.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa