Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa Ametoa siku mbili kuanzia tarehe 19-21 Januari, 2023 kwa Wazazi ambao hawajapeleka watoto wao Shuleni kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanapelekwa shuleni.
Amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya umaliziaji wa vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Dr. Mpango na Ikambi mwishoni mwa mwezi Januari, 2023.
Aidha Kanali Mallasa amewataka Watendaji wa Kata kuhakikisha wazazi wanawapeleka watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwani hakuna sababu yakuendelea kukaa na watoto nyumbani hali yakuwa madarasa yapo tayari. Ameendelea kusema kwa mzazi ambae ataendelea kukaidi kumpeleka mtoto wake shuleni hatua za kisheria zichukuliwe ikiwemo kuwafikisha mahakamani.
Mkuu wa Shule ya sekondari Dr.Mpango Boniface Kayombo amesema kuwa upatikanaji wa madarasa hayo yatasaidia kukuza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kwani kabla ya kupatikana kwa madarasa hayo hali ilikuwa ngumu.
Edga Dennis Abdallah Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Dr.Mpango amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwakuwajengea Shule karibu kwani walikuwa wanatembea umbali mrefu ambao ulikuwa unasababisha kutofika shule na badala yake kuishia njiani.
Naye Safina John Mabano Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Dr.Mpango ameishukuru Serikali kwa kujenga shule karibu kwani walikuwa wakikutana na vikwazo vingi hivyo kuahidi kufaulu katika masomo yao.
Fredrick Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Dr.Mpango amewaomba wazazi kuonyesha ushirikiano wa kuwapeleka watoto shule ili waweze kutimiza ndoto zao kwani wazazi wamekuwa wakiwanyima haki ya kupata elimu.
Wakazi wa Kijiji cha Kazilamihunda iliyopo katika kata ya Kasanda wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea miradi ya maendeleo ikiwemo Shule hivyo wameahidi kuendelea kushirikiana na Walimu pia kuendelea kutoa Elimu kuhakikisha wanapeleka watoto wao shule waweze kupata Elimu itakayo wasaidia baadae, vilevile wamewashauri wazazi wenzao ambao bado hawajapeleka watoto shule na kuacha kuwaficha watoto badala yake kuwatuma kwenda kufanya kazi za ndani.
Hadi sasa wazazi nane (8) Wamefikishwa ofisi ya Kata ya Kasanda kutoa maelezo ya sababu za kushindwa kuwapeleka watoto wao shule kuripoti.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa