Wazee 60 wa kata ya Nyamtukuza wamepatiwa kadi za matibabu iCHF zilizolipiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri katika kusherehekea siku ya wazee iliyoadhimishwa Jumatatu Oktoba 2, 2023.
Diwani wa kata ya Nyamtukuza Mhe.Abdallah Rajabu Maghembe ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo ameeleza kuwa Mzee wa leo ndiye kijana wa jana na kijana wa jana ndiye mzee wa kesho.
Aidha amewaasa wazee kuendelea kuwa mfano na walimu wazuri kwa vijana ili kuendelea kujenga taifa imara na lenye upendo na furaha katika jamii wanazoishi.
Naye Afisa Ustawi Bi.Epheta Msiga akiongelea Kauli mbiu ya siku hii "Uthabiti wa wazee kwenye dunia yenye mabadiliko alisema, kauli mbiu hiyo ni uthibitisho kuwa Taifa la Tanzania linalongozwa na Rais Dr.Samia Suluhu Hassan linajali na kutambua umuhimu wa wazee katika nchi hii leo na baadaye ndiyo maana Mkurugenzi ametoa kadi za ICHF kwa wazee na si kundi lingine katika jamii na kuongeza kuwa siku hii ni siku kubwa na yenye umuhimu kwa taifa hili.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa