Wilaya ya Kakonko yapokea tani 64 za mbolea ya Ruzuku kwa ajili ya kugawa kwa wakulima ambao tayari wamejiandikisha kwenye mfumo.
Akitoa taarifa hiyo katika kikao cha tathmini ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 kilichofanyika siku ya Alhamisi tarehe 20 Oktoba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dr.Godfrey Kayombo ameeleza kuwa tayari wakala aliyepangiwa kugawa mbolea Wilayani Kakonko amefika kwa ajili ya kugawa mbolea hiyo katika vituo ambavyo atapangiwa.
Dr.Godfrey Kayombo aliwasisitiza Wananchi waliojiandikisha kufika wenyewe Wilayani kuchukua mbolea hiyo ya ruzuku kwa bei ya Tshs.70,000 kwa mfuko kulingana na mahitaji waliyoyataja wakati wanajisajili.
Akihoji utaratibu utakaotumika katika ugawaji wa mbolea ya ruzuku katika kata, Diwani wa Kata ya Kasanda alihoji namna wananchi watakavyofikishiwa mbolea hiyo katika kata zao.
Mwenyekiti wa Chama Tawala (CCM) Saamoja Ndilaliha alisisitiza umuhimu wa Wananchi kufikishiwa mbolea katika kata zao na kushauri vituo visajiliwe kwa kila kata ili kuweza kugawa mbolea hiyo kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa