Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko anayo furaha kutangaza nafasi 22 za ajira ya kudumu kwa watanzania wote wenye sifa stahiki ikiwemo Katibu Muhtasi Daraja la III nafasi 04, Dereva Daraja la II nafasi 04, pamoja na Mtendaji wa Kijiji daraja la III nafasi 14. Nafasi za ajira hizi zinatokana na kibali cha ajira kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kwa barua yenye Kumb.FA.97/228/01/9 ya tarehe 13 Mei, 2022. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30/06/2022 saa tisa alasiri.Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa kutumia anuani ifuatayo;
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 03.
KAKONKO.
NB: Tangazo hili linafuta Tangazo lenye Kumb.Na.HW/KNK/PF/S.40/6/143 la tarehe 23/05/2022
Kwa maelezo zaidi Rejea tangazo la ajira hapo chini.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa