Baraza la Madiwani Wilayani Kakonko limeidhinisha bajeti ya bilioni 26.8 kutumiwa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ikilenga kupandisha vyeo watumishi 526,kuajiri watumishi wapya 174, kuwajengea uwezo watumishi na waheshimiwa madiwani, ununuzi wa gari la taka pamoja na kuelekeza 20% ya mapato sawa na milioni 247 kwa shughuli za maendeleo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri, Ndaki Stephano Mhuli wakati akiwasilisha bajeti kwa Waheshimiwa Madiwani katika mkutano maalum wa kujadili bajeti ya mwaka 2025/2026 akishirikiana na Afisa Mipango katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Jana Jumatano, Februari 12, 2025.
Mkurugenzi Mtendaji Ndaki amefafanua kuwa bajeti imelenga kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi kwa sekta ya elimu na Afya hivyo wamelenga kuajiri walimu wa shule za msingi 82 na wahudumu wa afya 43.
Aidha Tshs,752,720,000 zimetengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi na Waheshimiwa madiwani, Tshs,220,000,000 zimelenga kununua gari la taka ili kuondoka changamoto ya taka na Tshs.247,884,000 ambazo ni 20% ya mapato ya ndani ya Halmashauri zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ambapo Tshs.123,942,000.00 zitatumika kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu wakati Tshs.123,942,000.00 zitatumika kujenga vibanda vya biashara katika soko kuu la Kakonko.
Akiwasilisha bajeti kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, Afisa Mipango wa Halmashauri Ndaki Stephano Mhuli ameeleza kuwa Tshs.1,007,738,480 zitatumika kwa ajili ya kupandisha vyeo watumishi 526 kutoka Idara na Vitengo 18 ambapo wengi kati yao ni waalimu wa elimu msingi ambao ni 286, waalimu wa sekondari 82 pamoja na Wataalamu wa Afya 123.
Wawakilishi wa Wananchi kutoka kata 13 za Halmashauri wameoneshwa kuridhishwa na bajeti hiyo wakileleza kuwa imekidhi matarajio yao ya muda mrefu.
Mheshimiwa Augustino Linze, Diwani wa kata ya Kakonko ameshukuru kwa bajeti iliyowekwa kwa Kata ya Kakonko akitolea mfano ununuzi wa gari la taka kwani taka zimekuwa ni kero kwa wakazi wa Kakonko na kueleza kuhusu ujenzi wa shule ya msingi Mbizi ambayo imekuwa ni kilio kikubwa kwa wakazi wa kijiji cha Mbizi.
“Bajeti hii kwa kata ya Gwanumpu itatusaidia kununua mashine ya X- Ray na kujenga wodi ya wanawake wakati kwa sekta ya elimu tuniashukuru Serikali inayoongozwa na Rais Sami Suluhu Hassan kwa kutuwezesha kujenga shule mpya ya Sekondari Bukirilo hivyo kupitia bajeti hii tutajenga madarasa 04 katika shule shikizi itakayoitwa Kitagura ikitokea shule mama ya msingi Bukirilo yenye zaidi ya wanafunzi 1000”, Alieleza Mheshimiwa Toyi Butono, Diwani wa kata ya Gwanumpu.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa