Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Hosea Ndagala amekabidhi mabati 280 kwa wastaafu 14 kwa niaba ya kamati tendaji ya chama cha waalimu wilaya ya Kakonko (CWT) kwa mara ya kwanza tangu chama hicho kuanzishwa.
Akikabidhi mabati hayo kwa wastaafu katika hafla iliyofanyika katika ofisi za CWT wilayani Kakonko hivi karibuni, mgeni rasmi Col.Hosea amewapongeza wastaafu hao na kuwasisitiza kutumia zawadi waliyopewa kukamilisha nyumba zao au kuanzisha biashara.
“Niwapongeze na kila la kheri kwenda kuanza maisha mapya na mazuri, huu ni mwanzo mzuri kama hujamalizia kibanda kamalizie kama tayari ni vizuri kujenga kibanda cha biashara au kufuga”, alisema mkuu wa wa Wilaya.
Aidha amewasisitiza waalimu kujitoa kwa kuwa sehemu ya mwanafunzi na kuwaomba watumishi wanapokuwa kazini wajiandae kustaafu kwani kustaafu siyo mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mengine uraiani kwani fursa ni nyingi.
Col.Hosea Ndagala amesisitiza changamoto zisikatishe tamaa katika kufanya kazi kwani serikali inatua changamoto moja hadi nyingine na kuomba ushirikiano udumishwe ndani ya chama cha waalimu. Aidha ameomba chama cha waalimu kuendelea kutoa zawadi kwa wastaafu.
Mwenyekiti wa halmashauri mhe.Juma maganga ambaye alikuwa ameambatana na mgeni rasmi alipongeza chama cha waalimu kwa kutoa zawadi kwani kitendo hicho kitawajengea uwezo waalimu ambao wapo kazini wakijua kuwa wataendelea kupata huduma hata baada ya kustaafu.
Hata hivyo mwenyekiti wa chama cha waalimu wilaya ya Kakonko Tumaini Daniel amewaomba waalimu wastaafu kuwakumbusha waalimu waliopo kazini kufanya kazi na kuiomba halmashauri itenge bajeti ya kuwarudisha wanapotoka wastaafu baada ya kustaafu na Halmashauri iwaingize waalimu kwenye bajeti ya 2018/19 ili wapande madaraja kwani kuna waalimu zaidi ya 400 wanaotakiwa kupanda madaraja.
Mwalimu Masuhuko mstaafu aliyekuwa anafundisha shule ya msingi Bukiriro ameleza kufurahishwa na zawadi iliyotolewa na CWT kwa mara ya kwanza na kuahidi kwenda kukamilisha nyumba yake.
Aidha mwalimu Msitu Mninga Lameck mstaafu kutoka shule ya msingi Kabingo Katanga amewasisitiza waalimu wawe na wito wa kufanya kazi na wasipende malipo.
Hafla ya kuwakabidhi mabati 20 kila mstaafu kwa mara ya kwanza imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko ambaye alikuwa mgeni rasmi Col.Hosea Ndagala, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Juma Maganga, Afisa Elimu Msingi Wilaya Mwl.Joseph Mutahaba, kamati tendaji ya CWT na waastaafu husika.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa