Mafunzo hayo yameanza siku ya Jumatatu tarehe 11 Desemba, 2023 na yanatarajiwa kukamilika Jumamosi tarehe 16 Desemba, 2023.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuongozwa na Afisa Utumishi Bi.Hidaya Yusuph ambaye amewasisitiza Watumishi kuzingatia mafunzo hayo kwani upimaji wa utendaji wao wa kazi utafanyika kwenye mfumo wa PEPMIS na PIPMIS.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora bwana Priscus Tairo ameeleza kwa sasa mtumishi kupitia anuani ya www.ess.utumishi.go.tz mtumishi anataweza kujisajili na kupata huduma mbalimbali ikiwemo uhamisho, salary slip na huduma ya mikopo.
Aidha ataweza kutumia mfumo wa PEPMIS kupimwa utendaji wake wa kazi baada ya mkuu wa idara husika kuingiza malengo na mtumishi kupewa majukumu ya kutekeleza.
Mafunzo hayo yamehusisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa kata, Maafisa Elimu kata na maafisa Tarafa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa