Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Ndaki Stephano Mhuli amekabidhiwa cheti cha usajili wa kampuni ya Halmashauri na Mwanasheria wa Halmashauri siku ya Jumatatu Oktoba 30, 2023.
Tukio la makabidhiano ya cheti cha usajili limefanyika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji likishuhudiwa na Menejimenti ya Halmashauri wakati wa kikao cha asubuhi (morning glory) ambapo walimpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa hatua hiyo iliyofikiwa.
Kampuni ya Halmashauri imesajiliwa rasmi tarehe 20.10.2023 na BRELA kwa jina la Kakonko Development Company Limited ambapo namba za usajili ni 169494487.
Hii ni kufuatia timu iliyoteuliwa na Mkurugenzi mtendaji akiwemo Mwanasheria wa Halmashauri, Qeenity Temu na Mchumi Festo Basugoya kufuatilia mchakato wa uanzishwaji wa kampuni ambao ulikamilika Oktoba 20, 2023.
Kampuni hiyo imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya makampuni namba 12 ya mwaka 2002 ikilenga kuendesha miradi kwa faida.
Kakonko Development Company Limited itaanza kuendesha mradi wa ufyatuaji wa tofali ambapo tayari Kijiji cha Kanyonza kama mbia (partner) kimetoa hekari 10 kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiwanda na uzalishaji wa tofali unaendelea.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndaki Stephano Mhuli, kampuni hiyo itaendelea kujitanua na kusimamia miradi mbalimbali ya Halmashauri itakayoanzishwa hapo baadaye ikiwemo kilimo cha parachichi katika eneo la Mtendeli.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa