Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, amewataka watumishi Wilayani Kakonko kutumia muda wao katika kuwahudumia wananchi na kufanya kazi kwa ushirikiano na uaminifu katika kutoa huduma kwa wananchi.
Amesema hayo Ijumaa Disemba 15, 2023, alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi ndani ya Wilaya ya Kakonko.
Andengenye amewaomba watumishi kutumia muda wao katika kuwahudumia wananchi na kuendelee kutangaza kazi za maendeleo zinazofanyika kwani kazi hizo ni za wananchi kwa ajili ya kuwaondolea changamoto hivyo ni muhimu wananchi wazifahamu.
Aidha ameendelea kutoa rai kwa watumishi kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kuisaidia Serikali iendele kubaki kwenye nafasi yake kwani kufanya hivyo watakuwa wamemuheshimisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye kiongozi mkuu wa serikali wanayoitumikia.
‘’Tuendelee kufanya kazi zetu kwa uadilifu na uaminifu kwa sababu Imani huzaa Imani tumeaminiwa kwenye haya majukumu yetu alietuamini tumurudishie Imani kwa kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uadilifu,’’ Alisema Thobias Andengenye.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Ndaki Stephano Mhuli, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya kuendeleza miundombinu mbalimbali ndani ya Wilaya ya Kakonko ikiwemo miundombinu ya Elimu Afya, Maji, Umeme pamoja na Barabara.
Ameendelea kusema zaidi ya Billioni moja na Milioni mia mbili zimetumika katika kujenga miundombinu ya elimu kwa kata ya Nyamtukuza.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa