Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye kwa kushirikiana na kamati ya Usalama ya Mkoa amefanya ziara Wilayani Kakonko na kukagua jumla ya miradi 6 itakayotembelewa na Mwenge wa uhuru tarehe 05.10.2022.
Miradi iliyotembelewa ni Kituo cha Afya Mugunzu, Klabu ya Wapinga rushwa katika shule ya Sekondari Gwanumpu, Mradi wa Maji katika Kijiji cha Nyakayenzi Kata ya Kasuga, Zahanati ya Kihomoka inayojengwa kwa mapato ya ndani, Shule ya Sekondari ya Wasichana Kakonko na Kikundi cha Vijana Tuinuane kilichopo katika kata ya Kanyonza.
Mkuu wa Mkoa Thobias Andegenye pamoja na wajumbe walioambatana naye wamesisitiza marekebisho yafanyike katika miradi husika mfano marekebisho ya milango ambapo ameelekeza mlango katika bweni la Wasichana katika shule ya Wasichana ifunguke kwa nje kwa ajili ya usalama wa Wanafunzi pindi ajali ya moto inapoweza kutokea.
Mkurugenzi Mtendaji Ndaki Stephano Mhuli ameahidi kufanya marekebisho hayo na kueleza shule hiyo ilianzishwa mahusususi kwa ajili ya kupunguza vitendo vya wanafunzi wa kike kuacha shule ambapo kwa sasa kila kata wanachukuliwa wanafunzi sita waliofaulu vizuri katika masomo yao.
Aidha katika shule ya Sekondari Gwanumpu wanafunzi wa klabu ya wapinga rushwa wamehimizwa kuendelea na mapambano dhidi ya Rushwa na kujiandaa wakati wote kupinga vitendo vya rushwa.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa tarehe 05.10.2022 Wilayani Kakonko kisha unatarajiwa kukabidhiwa katika Mkoa wa Kagera ambapo kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru itakuwa ni tarehe 14.10.2022 ambapo Mwenge wa Uhuru utazimwa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa