Mwenge wa Uhuru umezindua na kutembelea miradi 5 yenye thamani ya shilingi 552,199,651.00 Wilayani Kakonko Aprili 16 mwaka huu.
Akizungumza wakati anakabidhi mwenge wa Uhuru Wilayani Kibondo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema Mwenge umezindua na kutembelea miradi 5 yenye thamani ya shilingi 552,199,651.00 ukiwemo mradi wa kituo cha afya cha Nyanzige wenye thamani ya shilingi 271,299,651, mradi wa maji wa Kijiji cha Kasanda tsh 227,000,000.00, Jengo la Kitega Uchumi Kasanda 20,000,000.00, Vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Mganza shilingi 33,900,000.00 na uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa uliofanyika katika shule ya msingi Kinonko.
Akitoa ujumbe wa Mwenge Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru, Charles Kabeho amesema ujumbe wa Mwenge mwaka huu ni elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu na pamoja na kauli mbiu hiyo mbio za mwenge wa uhuru zitaendelea kuhamasisha jamii kupambana na rushwa, mapambano dhidi ya ukimwi na mapambano dhidi ya malaria na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
Mwenge wa uhuru umewasili mkoa wa Kigoma ukitokea mkoani Kagera ambapo unatarajiwa kuzindua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi 50 yenye tamani ya shilingi bilioni 12.6 katika miundombinu ya maji, afya, elimu.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga akipokea mwenge kutoka kwa Mkuu mkoa wa Kagera katika Kijiji cha Nyamtukuza wilaya ya Kakonko alisema mwenge huo utakimbizwa katika Halmashauri nane na utaanza kukimbizwa katika wilaya ya Kakonko na kumuomba kiongozi wa mbio za mwenge Charles Kabeho, mwenge huo utumike kuhimiza wakimbizi walioko Tanzania kurejea nchini kwao kwa hiyari kwa kuwa nchi hiyo kwa sasa ina amani na ni tulivu.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa