Afisa Mipango Michael Faraay akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano mbele ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongzoi na Mipango waliotembelea ujenzi huo eneo la Kanyamfisi tarehe 18 Aprili, 2023.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Mhe.Fidel Nderego akihoji kuhusiana na maendeleo ya Ujenzi wa Ukumbi wa Halmashauri ambao upo hatua ya msingi na kupandisha nguzo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Ndaki Stephano akitoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa Vyoo na ukarabati wa madarasa katika shule ya Sekondari Kashoza iliyopo kata ya Nyabibuye baada ya kamati ya Fedha kufanya ziara shuleni hapo Aprili 18, 2023.
Wajumbe wa kamati ya Fedha wakijadiliana kuhusu ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari Kashoza iliyopo kata ya Nyabibuye baada ya kufanya ziara shuleni hapo Aprili 18, 2023.
Diwani wa kata ya Nyabibuye Mhe.Januari Mbanyi akitoa maelezo ya hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa vyoo shule ya sekondari Kashoza kamati ya Fedha ilipotembelea shuleni hapo Aprili 18. 2023.
Ujenzi wa nyumba ya waalimu (2 in 1) ikiwa katika hatua ya ukamilishaji katika shule ya Sekondari Ndalichako iliyopo kata ya Muhange kwa Gharama ya Tshs.114,683,972.75 kwa nyumba mbili
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Fidel Nderego akihoji kuhusiana na Ujenzi wa nyumba 2 za waalimu katika shule ya Sekondari Ndalichako iliyopo kata ya Muhange baada ya kamati ya Fedha kufanya ziara shuleni hapo Aprili 18, 2023.
Wajumbe wa kamati ya Fedha wakipata maelezo kuhusu ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Malenge iliyopo kata ya Rugenge iliyogharimu TshsTshs.41,540,000 baada ya kutembelea shuleni hapo Aprili 18, 2023.
Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, kutengenezwa kwa madawati 30, meza 2, viti 2 na kuingiza umeme kwenye madarasa 6 na ofisi moja katika shule ya msingi Malenga iliyopo kata ya Rugenge umekamilika kwa gharama ya Tshs.41,540,000.
Kamati ya Ujenzi wa Zahanati ya Rusenga iliyopo kata ya Gwanumpu wakitoa maelezo ya hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa wajumbe wa kamati ya Fedha waliofanya ziara Kijijini hapo Aprili 18, 2023.
Wajumbe wa kamati ya Fedha wakihoji kuhusiana na hatua ya Utekelezaji wa ujenzi wa Zahanati ya Rusenga iliyopo kata ya Gwanumpu baada ya kutembelea kijijini hapo Aprili 18, 2023.
Wajumbe wa kamati ya Fedha wakipata maelezo kuhusiana na Ujenzi wa shule ya Sekondari Katanga iliyopewa Ts470,000,000 na tayari shule hiyo imefunguliwa ikiwa na wanafunzi 120.
Ndaki S.Mhuli, Mkurugenzi Mtendaji akieleza kuhusiana na Ujenzi wa nyumba mbili za Wakuu wa Idara eneo la Rukenamaguru wakati kamati ya Fedha ilipofanya ziara hapo Aprili 19, 2023.
Ujenzi wa wodi 3 (Wodi ya Watoto, Wanawake na Wanaume katika hospitali ya Wilaya ukiwa unaendelea kwa gharama ya Tshs.750,000,000
Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kakonko Dr.Tinuga Cosmas akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa wodi tatu kwa Wajumbe wa kamati ya Fedha walipotembelea hospitali ya Wilaya iliyopo Kijiji cha Itumbiko, Kata ya Kakonko Aprili 19,2023.
Wajumbe wa kamati ya Fedha watembelea kichomea taka katika hospitali ya Wilaya ya Kakonko.
Wajumbe wa kamati ya Fedha wakipata maelezo kuhusu mashine ya X-ray katika hospitali ya Wilaya ya Kakonko.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Kakonko Anatoria Nkabo akitoa maelezo kuhusu Ujenzi wa bweni la Wasichana unaotekelezwa kwa thamani ya Tsh142,934,332 kupitia ufadhili wa TEA baada ya Kamati ya fedha kutembelea shuleni hapo Aprili 19, 2023.
Mwenyekiti wa halmashauri Mhe.Fidel Nderego akitoa maelekezo baada ya kupata taarifa ya ujenzi wa bweni la Wasichana katika shule ya Sekondari wasichana Kakonko kamati ya Fedha ilipotembelea hapo Aprili 19, 2023.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha wakikagua Ujenzi wa madarasa 8 katika shule ya Sekondari Wasichana Kakonko walipotembelea Aprili 19, 2023.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa